NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) imetafsiri sheria 300 kati ya sheria 446 kutoka  lugha ya kiingereza kuwa kiswahili katika  kipindi cha miezi sita cha mwaka 2025 ambapo Sheria 146 zilizozobakia zinatarajiwa kutafsiriwa katika bajeti ya mwaka fedha 2025/2026 ili wananchi wanapozisoma wazielewe.

Ameyasema hayo leo Julai 11,2025 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas ndumbaro  alipotembelea banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) katika Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (Sabasaba).

Aidha Dkt Ndumbaro amesema ofisi ya Mwandishi mkuu wa  Sheria imekuwa msaada mkubwa kwa mahakama nchini kwa kutimiza wajibu wake  katika kuandaa Sheria ambazo zimefanyiwa urekebu ili zitumike katika wakati sahihi.

Dkt Ndumbaro ameongeza kuwa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD
ina wajibu mkubwa  katika zoezi la kutunga na kuchakata sheria za nchi,ikiwa  ni pamoja na kuzitafsiri kwa lugha ya kiswahili ili zieleweke.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...