Mwanzo Mwema ni mradi wa miaka minne unaofadhiliwa na shirika la GAVI, unaolenga kuboresha afya ya watoto kupitia chanjo iliyoimarishwa nchini Tanzania.

Mradi huu unalenga hasa kuongeza uchanjanji wa chanjo za awali za watoto (RoutineImmunization - RI) na chanjo dhidi ya virusi vya HPV (Human Papillomavirus), hasa katika jamii zisizohudumiwa ipasavyo na maeneo ambayo ni vigumu kufikika.

Katika kitovu cha Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, safari ya Scholastica ilianza yenye lengo la kuwawezesha wasichana katika jamii yake. Akiwa mshiriki wa Kamati ya Ushauri wa Vana (YAP), alipata malengo kupitia programu ya Mwanzo Mwema ya Girl Effect Tanzania.

Kile kilichoanza kama maono, kiligeuka kuwa nia yenye nguvu ya kubadilisha maisha kwa njia ambazo hakuwahi kufikiria.

Akiwa kana anejitolea kwenye jamii, Scholastica hakusambaza tu nyenzo za kujifunzia lakini alivigeuza kuwa nguzo ya maisha ya kila siku. Wakati wa kampeni maalum za afya kwenye jamii, aligundua haraka pengo muhimu: wazazi wengi, hasa akina mama walioko vini, hawakuweza kusoma vifaa alivyokuwa akivitoa.

Badala ya kuruhusu changamoto hii kuzuia upatikanaji wa taarifa muhimu za uokoaji maisha, Scholastica alikuja na suluhisho rahisi lakini lenye nguvu alianza kusoma machapisho hayo kwa sauti. Sauti yake ikawa daraja kati ya maarifa ya afya na wale walezi waliohitaji elimu hiyo zaidi. Kupitia vipindi vyake, hata wale ambao hawajawahi kusoma walielewa umuhimu wa chanjo na ratiba zake.

Mafanikio yalikua wazi. Jamii ambazo hapo awali zilionekana kuwa ngumu kufikika zilianza kushiriki. Wazazi walipata maarifa zaidi, na viwango vya chanjo za watoto chini

ya miaka mitano viliongezeka, na kuhakikisha watoto wengi zaidi wanalindwa dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Ubunifu wa Scholastica haukuishia kuelimisha tu uliwezesha jamii, ikithibitisha kwamba maarifa hayapaswi kutolewa katika maandishi pekee.

Leo, Scholastica si tu mtetezi wa afya ya watoto yeye ni mshauri, mjasiriamali, na mfano wa kuigwa kwa wasichana wengi ndani ya Masasi. Safari yake inathibitisha kwamba vana wanapowezeshwa, wanakua sio washiriki tu bali huwa wanatengeneza,wanaongoza, na kubadilisha jamii zao.

Akikumbuka uzoefu wake, Scholastica anasema: “Mafunzo ya ujasiriamali yalinibadilisha kabisa. Yalinipa zana za kugeuza shauku yangu kuwa biashara inayoendelea na kunipa ujasiri wa kuwaongoza watu wa kwetu kuelekea kujitegemea kiuchumi. Tumaini langu ni kwamba kila kana atambue uwezo wake kama nilivyofanya mimi.”

Uongozi wake ni ushahidi wa kile kinachowezekana pale ambapo wasichana wanapewa uwezo si tu wa kuota, bali wa kutenda.

Safari ya Scholastica inaonyesha nguvu ya kuwaamini na kuwawezesha vana kuongoza. Mchango wake ni kielelezo cha kina kinachotokea pale vana wanapopewa nyenzo, jukwaa, na imani ya kuleta mabadiliko.

Hata hivyo, bado jamii nyingi hazina upatikanaji wa taarifa muhimu za afya, na vana wengi wenye akili nyingi bado hawajapewa nafasi ipasavyo wakisubiri nafasi ya kung'ara.

Kupitia uwekezaji endelevu kwenye miradi inayoongozwa na vana kama Mwanzo Mwema, tunaweza kuongeza suluhisho kwenye jamii, kuziba pengo la usawa wa kiafya,na kuwawezesha kizazi kipya cha viongozi wenye mabadiliko walio tayari kushiriki, na zaidi kuongoza katika mstari wa mbele.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...