Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KAMPUNI ya Strategis Insurance imezindua bidhaa mpya ya Bima ya Matrekta inayolenga kumlinda mkulima dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza wakati wa shughuli za kilimo, hatua inayochukuliwa kama sehemu ya kuimarisha ustawi wa mkulima na kukuza mnyororo wa thamabi katika sekta hiyo.
Bima hiyo inalenga kuwalinda wakulima na vifaa vyao vya kulimia na kuvunia, sambamba na kutoa bima kwa madereva wa matrekta pindi wanapokumbwa na ajali au changamoto nyingine kazini.
Uzinduzi wa bima ya matrekta imezinduliwa Julai 15,2025 jijini Dar es Salaam na kwamba bima ya matrekta itapatikana mikoa yote nchini,hivyo wakulima wameombwa kuchangamkia bima hiyo ambayo ni maalum kwa ajili yao.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bima ya matrekta ,Ofisa Mkuu wa Bima ya Ajali katika kampuni hiyo Jabir Kigoda amesema wamekuja na bima hiyo kwasababu wameona kilimo ni sekta ya kipekee inayohitaji kuangaliwa kwa namna ya kipekee.
“Kutokana na upekee wa sekta ya kilimo na inahitaji kuangaliwa kwa tofauti kidogo tukasema pia tuongeze mnyororo wa thamani katika kilimo na ndio wazo la kuja na bima ya trekta ikazaliwa.
“Bima yetu hii itawafikia wakulima ,tunafahamu kilimo hakifanyi mjini ingawa matrekta mengi yanauzwa mjini, kwahiyo tulichofanya cha kwanza ni kuweka mkakati wa kushirikiana na wadau namba moja ambao wanauza matrekta ambao ndio wanafahamu na wanaweza kuwafikia wakulima kwa urahisi zaidi.
“Pia tumeshirikiana na mabenki kwasababu yenyewe ndio yanaweza kutoa mikopo kwa wakulima ambao wanakwenda kuchukua hayo matrekta na kwenda kuandaa kilimo kuweza kufikia malengo yao.”
Ameongeza kuwa mkakati mwingine katika kuhakikisha bima ya matrekta inafika kwa wakulima wanashirikiana na vyama vya ushirika vilivyopo katika mikoa mbalimbali huku akisisitiza uzuri wao wana matawi yao karibia kanda zote nchini Tanzania.
“Tunayo matawi Mwanza,Dodoma,Dar es Salaam ,Zanzibar na Arusha ambako inajumuisha mikoa ya kaskazini na siku za karibuni tutakuwa na tawi Mbeya.Hivyo kote huko bima ya matrekta itakuwa inapatikana baada ya leo kuizindua rasmi.”
Amesisitiza kwahiyo kila kanda wameweka kituo chao cha mauzo ili kuweza kutoa elimu ya kueleza bidhaa tofauti hasa hiyo bima ya matrekta.Kwahiyo tunaamini kwa kutumia mkakati huo watawafikia wateja wao.
Aidha amesema wanawashukuru wateja kwani wamekuwa nao pamoja muda mrefu na wameendelea kuwaamini kwa kila hatua,hivyo hatua hiyo ya kuzindua bima ya matrekta wataiunga mkono kama ambavyo wamekuwa wakifanya siku zote.
“Tutaendelea kufanya vizuri kama ambavyo tumekuwa tukifanya ,kuna sababu kwanini tunaongoza kwenye soko hili la bima .Hakuna mtu anayependa kwenda kukatia bima kwenye kampuni ambayo itampa usumbufu wakati wa madai.
“Kwahiyo tumekuwa kinara katika soko la bima kwasababu wateja wetu wanaamini huduma zetu ,tutaendelea kutoa huduma zetu na tutazifanya kuwa bora zaidi ,tutaendelea kutengeneza bidhaa ambazo zitakwenda kukidhi mahitaji yao.Kwa mfano mmoja mzuri ni huu wa huduma ya Bima ya trekta ambayo tunaamini inakwenda kukidhi mahitaji yao,”amesema Kigoda.
Hata hivyo amesema kampuni yao kabla ya kutoa bidhaa huwa wanafanya tafiti kuangalia kitu gani kinatakiwa,hivyo wanaangalia tija ambayo bidhaa italeta kwa mteja,pia wanaangalia kama nchi inakwenda kunufaika vipi na hiyo bidhaa ambayo tumeingiza sokoni pamoja na kampuni zinakwenda kufaidika vipi.
Kwa upande wake Dk.Flora Minja ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Strategis Insurance, amesema wamekuwa na mikakati ya kuhakikisha elimu ya bima inawafikia Watanzania wote ili huduma mpya kama huduma ya bima ya matrekta ziweze kueleweka na kutumika kwa ufanisi.
Amefafanua kwamba lengo likiwa ni kumpa mkulima uhuru zaidi wa kufanya kilimo bila hofu ya hasara kubwa zinazoweza kutokea kutokana na majanga yasiyotabirika huku akisisitiza wamekuwa wakitoa elimu ya bima kupitia matawi ya kampuni hiyo yaliko katika mikoa mbalimbali .
“Uelewa wa bima kwa wananchi uko chini lakini sisi kama Kampuni kwa kushirikiana na wadau wengine lazima tushirikiane kutoa elimu kuhusu bima. Pia tunafanyakazi kwa ukaribu na TIRA ambayo yenyewe ndio msimazi anayewaongoza katika kuongeza uelewa wa umuhimu wa bima
“Mwito wangu kwa wadau wengine wa bima tunatakiwa kuongeza idadi ya watu wanaotumia bima hapa Tanzania na lazima tushirikiane maana kampuni moja moja haitaweza kufika pale tunatarajia ,kwahiyo lazima tushirikiane kueneza habari hizi ili tuweze kuwafikia walengwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...