MAOFISA na askari wa mbwa wa vita kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliyohitimu mafunzo ya mbwa wa vita wametakiwa kuzidi kujiendeleza katika mafunzo waliyoyapata ili kuendeleza weledi walioupata katika kozi hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Polisi wa Jeshi kwa Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Brigedia Jenerali Abubakari Charo wakati ufungaji wa mafunzo ya ubobezi kwa maafisa na askari waliyohitimu mafunzo hayo katika Kikosi cha Mbwa vita 1K9 cha JWTZ.
Amesema muhimu kwa maofisa na askari hao kuhakikisha wanajiendeleza katika mafunzo waliyoyapata Ili kuendeleza weledi walioupata katika kozi hiyo hasa katika masuala ya ulinzi wa amani
Aidha Brigedia Jenerali Charo amempongeza Mkuu wa Kikosi cha Mbwa vita Luteni Kanali Meshark Kibubu kwa juhudi anazozionyesha katika kusimamimia mafunzo hayo kwa maafisa na askari wa mbwa vita katika jukumu lao la msingi la ulinzi wa nchi ikiwa ni pamoja na kushiriki operesheni za ndani na nje ya nchi, uokoaji na ulinzi wa amani.
Naye Mkuu wa Kikosi cha Mbwa vita 1k9, Luteni Kanali Meshark Kibubu amesema kuwa anashukuru Makao makuu ya Jeshi na wahitimu wake wote kwa jinsi Jeshi linavyoweka kipaombele katika kuendeleza mafunzo ya mbwa vita ili kikosi kiweze kutekeleza dira na dhima ambayo ni kuwa kituo bora cha mafunzo kwa maafisa na askari na mbwa vita wa JWTZ wenye weledi, hodari, ujasiri na utayari wa kutekeleza majukumu ya JWTZ kitaifa na kimataifa.
Aidha. Kamanda kikosi 1K9 aliongeza dhima ya kikosi ni kufundisha maafisa, askari na mbwa vita Ili walitumikie Jeshi kikamilifu wakati wa amani na wakati wa vita pamoja na Kushiriki katika Ulinzi wa Amani katika nchi zenye machafuko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...