.jpeg)
Kupitia kliniki hiyo, FCC inalenga kuwapatia wafanyabiashara hawa taarifa sahihi na za faragha kuhusu sheria za ushindani na ulinzi wa watumiaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha ukuaji shirikishi wa uchumi unaozingatia usawa na haki katika soko.
Akizungumza Julai 4, 2025 katika banda la FCC, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Hadija Ngasongwa alisema kuwa taasisi hiyo inalenga kuwafikia zaidi ya washiriki 3,500 kutoka sekta mbalimbali za biashara ili kuwajengea uelewa utakaowawezesha kuendesha shughuli zao kwa kufuata sheria, huku wakijilinda dhidi ya ushindani usio wa haki.
“Kwa kliniki hii, tunawawezesha wajasiriamali wa kati na wadogo kuelewa haki zao kama watumiaji wa soko, lakini pia wajue wajibu wao kisheria. Hii ni hatua muhimu kwa ukuaji wao na mchango wao katika uchumi wa taifa,” alisema Bi. Ngasongwa.
Aliongeza kuwa FCC imekuwa ikiendesha kampeni mbalimbali za uelimishaji, pamoja na kufanya tafiti na ufuatiliaji wa mwenendo wa soko ili kudhibiti bidhaa bandia na uonevu wa kibiashara unaoweza kudhoofisha juhudi za wajasiriamali chipukizi.
Kwa mujibu wa Bi. Ngasongwa, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya kibiashara kwa kuweka mifumo rafiki kwa wawekezaji, hatua inayochochea ukuaji wa sekta binafsi hususan kwa vijana na wanawake wanaoingia kwenye biashara.
“Sheria zetu ni rafiki kwa wawekezaji na kwa wajasiriamali wanaochipukia. Tunataka kuhakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika uchumi bila vikwazo vya ushindani usio wa haki,” alisisitiza.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...