Kibaha, Julai 30, 2025: Katika uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika leo katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kwamfipa – Kibaha Mjini, wagombea Hawa Mchafu Chakoma na Mariam Ibrahim wameibuka vinara katika nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani.


Jumla ya wagombea wanane (8) waliingia kwenye kinyang'anyiro hicho, ambapo kura 2,108 zilipigwa huku kura halali zikiwa ni 2,103 na kura 5 zikiwa zimeharibika. Wapiga kura waliojitokeza ni 2,095.

Katika matokeo hayo:

● Hawa Mchafu alipata kura 802

● Mariam Ibrahim alipata kura 645

● Nancy Mutalemwa kura 449

Fatuma Uwesu (71), Irene Makongoro (52), Sifa Mwaruka (44), Rehema Issa (26), na Rehema Mssemo (7).

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi, zoezi hilo lilifanyika kwa amani na utulivu mkubwa, huku wajumbe wa CCM wakionyesha hamasa ya hali ya juu kuchagua wanawake watakaowakilisha mkoa huo bungeni.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Hawa Mchafu aliwashukuru wajumbe wa CCM kwa kuendelea kumuamini na kuahidi kuwa sauti ya wanawake na vijana wa Pwani haitazimika ndani ya Bunge.

“Nitashirikiana na kila mmoja wenu kuimarisha mshikamano, maendeleo ya kijinsia na ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya kitaifa,” alisema Hawa Mchafu.

Kwa upande wake, Mariam Ibrahim – ambaye ni miongoni mwa nyuso mpya zilizowika kwenye kinyang’anyiro hicho – alielezea furaha yake kwa kupewa fursa ya kuwakilisha kundi la wanawake na vijana wapya katika siasa za mkoa huo.

Zoezi hilo linaonesha msukumo wa CCM wa kuendeleza usawa wa kijinsia na kutoa nafasi kwa viongozi vijana, hasa wanawake, kushiriki katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia Bunge.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...