Na: Calvin Edward Gwabara – Dar es salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.
Hamza Johari ameitaka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria nchini (OCPD) kujitahidi
kukamilisha zoezi la ufasili wa sheria zote kwa lugha ya Kiswahili hasa za zile
za uchaguzi mkuu na kanuni zake ili zipatikane kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka
huu.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari akipokea zawadi kutoka kwa Bi. Mariam Possi alipotembelea banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria nchini (OCPD). |
Wito huo ameutoa wakati
alipotembelea Banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria nchini (OCPD) kwenye
maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya SABASABA yanayoendelea kwenye viwanja vya
Mwl Nyerere Jijini Dar es salaama na kutaka kujua mahitaji ya wananchi wayoleta
kwenye banda hilo ili waweze kuyafanyia kazi.
“Nafikiri tuendelee kuongeza
jitihada katika kazi yetu tunayoifanya ya kufanya ufasili wa sheria maana kwa kufanya hivyo tutawezesha
ufikiwaji wa haki kwa wananchi vizuri hasa hizi sheria za uchaguzi na kanuni
zake” Alisisituza Mhe. Johari.
Aidha ameipongeza Ofisi hiyo kwa
kazi nzuri wanayoifanya kwa kutoa elimu hiyo kwa umma kupitia maonesho hayo ya
sababsaba pamoja na kazi zingine wanazozifanya katika kutekeleza majukumu ya
ofisi hiyo waliyopewa kisheria.
Awali Mwandishi wa sheria kutoka
OCPD Bi. Mariam Possi alimueleza Mwanasheria Mkuu mambo muhimu ambayo wananchi
wanaofika kwenye banda hilo kupata maelezo na kujifunza masula ya mchakato wa
utungwaji wa sheria hadi kusainiwa na Rais, namna zoezi la Urekebu wa sheria
unavyofanyika na faida zake pamoja na ufasili wa sheria nchini unavyofanyika,
ulipofikia na umuhimu wake katika masuala ya utoaji wa haki kwa jamii.
“Katika kipindi chote ambacho
tumekuwa kwenye maonesho haya tunapokea wadau wengi wa sheria nchini pamoja na
wananchi wenyewe kutoka maeneo mbalimbali ambao wanataka kujua majukumu ya
Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na namna ambavyo wanaweza kuzipata sheria
zilizofanyiwa urekebu toleo la mwaka 2023 pamoja na hizi ambazo zipo kwenye
hatua ya mwisho za kufanyiwa ufasili kutoka lugha ya Kiingereza kwenda
Kiswahili” Alifafanua Bi. Poss.
Mwandishi huyo wa Sheri amesema
wanajitahidi kuwaelekeza michakato yote hiyo inavyofanyika kwa umakini lakini
kwa kuzingatia sheria na miongozo na kuwaahidi kuwa Serikali kupitia Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria wanaendelea
kutumia njia mbalimbali ambazo zitasaidia sheria hizo kuwafikia wananchi popote
walipo ili wazisome na kuzielewa na kusaidia jamii kupata haki zao na kujua
wajibu wao.
Kauli
Mbiu ya maonesho ya 49 ya Kimataifa ya SabaSaba ni “Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar
es Salaam ‘Sabasaba’ – Fahari ya Tanzania.”
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari akijisajili kidigital kwenye mfumo wa wananchi waliotembelea banda la OCPD kwenye maonesho ya sabasaba. |
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari akipata maelezo kutoka kwa Bi. Mariam Possi ambaye hayupo pichani wakati akisaini kitabu cha wageni bandani hapo. |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...