Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza kuanza kwa usajili wa mitihani ya 31 ya kitaaluma (Mid Session Examinations) itakayofanyika kuanzia tarehe 25 Agosti hadi 29 Agosti 2025, katika kituo kimoja kilichopo jijini Dodoma.


Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam tarehe 03 Julai 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Bw. Godfred Mbanyi, alisema kuwa usajili kwa ajili ya mitihani hiyo unafanyika kupitia tovuti rasmi ya usajili: https://registration.psptb.go.tz, na tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni 15 Agosti 2025.


Kwa mujibu wa Bw. Mbanyi, waombaji wa mitihani hiyo ni pamoja na Wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu na kati katika fani ya Ununuzi na Ugavi kwa ngazi za Astashahada, Stashahada, na Shahada kuanzia mwaka 2024 kurudi nyuma, ambao hawajawahi kufanya mitihani ya kitaaluma ya Bodi.


Pia amesema Wafanyakazi katika sekta binafsi na umma wanaojihusisha na kazi za Ununuzi na Ugavi lakini hawana cheti cha kitaaluma cha CPSP, Wahitimu wa fani nyingine wanaomiliki Stashahada, Shahada au Astashahada kutoka taasisi zinazoaminika na kutambuliwa na PSPTB, Watahiniwa waliomaliza ngazi mbalimbali za mitihani ya awali (Basic Stage II), msingi (Foundation Stage I & II), na taaluma (Professional Stages I–IV) ndani ya miaka mitano, kama inavyobainishwa kwenye Mtaala wa Kitaaluma na Watahiniwa wanaorudia baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali ndani ya kipindi cha miaka mitatu, kulingana na matakwa ya mtaala mpya.


Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa watahiniwa wanaorudia mitihani zaidi ya ngazi moja wanaruhusiwa kuunganisha ngazi mbili mfululizo (two consecutive blocs) kwa masomo yasiyopungua mawili na yasiyozidi sita, kulingana na ratiba ya mitihani ya 31.


Aidha, alieleza kuwa ada za mitihani zimechapishwa kwenye tovuti rasmi ya Bodi: www.psptb.go.tz, na kwamba ratiba ya mitihani mingine ya kawaida inayofanyika Novemba na Mei itaendelea kama kawaida.



Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Bw. Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa usajili wa mitihani ya 31 ya kitaaluma (Mid Session Examinations) itakayofanyika kuanzia tarehe 25 Agosti hadi 29 Agosti 2025, katika kituo kimoja kilichopo jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Bw. Godfred Mbanyi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Bodi hiyo katika Banda la PSPTB katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 49 yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...