Songea_Ruvuma.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma, Mrakibu wa Polisi Issa Milanzi, amewataka madereva wote mkoani humo kuhakikisha wanahakiki leseni zao kwa kufika katika ofisi za usalama barabarani ili kubaini uhalali wa leseni wanazotumia.
Amesema Lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha kila dereva anayeendesha chombo cha moto anakuwa na sifa stahiki kisheria,amesisitiza kuwa ni marufuku kwa dereva kutaja namba ya leseni badala ya kuwasilisha leseni halisi pindi anapoombwa na askari wa usalama barabarani.
Aidha, amesema kuwa madereva wote wanapaswa kutembea na leseni halisi (original) wakati wote wawapo barabarani, na si kutoa nakala (kopi), kwani kufanya hivyo ni kosa na kunaweza kupelekea dereva kutozwa faini.
Ameonya madereva wote wanaoendesha vyombo vya moto bila kuwa na leseni halali, akisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwa ni pamoja na faini, kufungiwa leseni au kupewa onyo kulingana na uzito wa kosa.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linaendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva ili kuwahimiza kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara pamoja na kuhakikisha kila mtumiaji wa chombo cha moto awe kapata mafunzo kutoka VETA na leseni ya daraja husika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...