
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na UNDP, imezindua nyaraka tatu muhimu za usimamizi wa maafa katika Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Nyaraka zilizozinduliwa:
Mpango wa Kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Wilaya (D-EPRP)

Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya Maafa (D-DRRS)
Ripoti ya Tathmini ya Vihatarishi, Uwezekano wa Kutokea na Uwezo wa kukbailian na maafa (RVCA)
📅 Uzinduzi umefanyika tarehe 23 Julai 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wananchi.

🎙️ Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Nyakia Chirukile:
> "Hii ni hatua muhimu kujenga mfumo wa utayari dhidi ya majanga kama mafuriko."

Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hosea Ndagalla, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa OWM:
> "Ni utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya 2022."

UNDP Tanzania kupitia Bw. Godfrey Mulisa:
> "Mpango huu ni sehemu ya kusaidia jamii kujenga upya maisha yao na kuwa imara zaidi."



#Maafa2025 #Sumbawanga #UtayariDhidiYaMajanga #UNDP #OWM

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...