Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amesema pamoja Serikali kufanya kazi kubwa hasa katika Sekta ya Afya ikiwemo vifaa,Dawa,Majengo na miundombinu na Watumishi lakini bado safari ya maendeleo katika Sekta hii huwa haiishi kutokana na watu kuongezeka na magonjwa kubadilika.

RC Senyamule amesema hayo leo Jijini Dodoma Julai 4,2025 katika hafla fupi ya kupokea Mashuka Mia tatu ya kuhudumia wagonjwa waliopo Mahospitalini katika Hospitali za Mkoa wa Dodoma yaliyotolewa na wana Ushirika wa Tanesco Saccos. 

Na kuongeza kuwa kutoka na uhitaji wa kila siku Serikali hata kama ingenunua Mashuka mengi kiasi gani bado yasingeweza kudumu siku zote kwani ingefika muda yangechakaa na kuhitajika mengine.

"Tunajua kuwa Serikali yetu chini ya Mhe Raisi imefanya kazi kubwa sana katika Sekta ya Afya,zipo Sekta zingine lakini katika Sekta ya afya imefanya makubwa kuanzia Vifaa,Majengo,Miundombinu,Watumishi na vitu vingine vingi, lakini tunafahamu kuwa bado safari hii ya maendeleo haina mwisho kila siku tunafanya lakini bado watu wanaongezeka na magonjwa yanabadilika kupelekea uhitaji wa kila siku katika baadhi ya maeneo".

"Kwahiyo mahitaji hayafiki mwisho hata siku moja,kwahiyo ukienda kwenye sekta ya afya unakuta kuna uhitaji mpya,mfano mashuka hata Serikali ikinunua mengi kiasi gani lakini baada ya muda yachakaa na kuhitajika mengine".

Aidha imepongeza Tanesco Saccos kwa mchango huo wa Mashuka ambao ni wa thamani na heshima kwa wana Dodoma utakaowagusa wagonjwa ambao watafika katika Hospitali za Mkoa huu wa Dodoma ambazo zitapewa mashuka hayo ambayo yataleta kumbukumbu nzuri, kwani fedha zilizotakiwa kununua Mashuka katika hospitali hizo sasa zitakwenda kununua Dawa na vifaa vingine.

Naye Mtendaji Mkuu wa Tanesco Saccos  Andrea Hilary amesema kuwa katika zoezi hili la kutoa mahitaji ya Mashuka katika Hospitali walipata Msukumo kwa kujua kuwa Sekta ya Afya ni kubwa na yenye uhitaji mwingi hivyo Serikali pekee haiwezi kujitosheleza pamoja na kufanya makubwa katika Sekta hiyo, kwani uhitaji ni wakila siku na kwa kuona hilo na wao waliona wanayo nafasi ya kufanya ili kuigusa jamii.

Na kusema walichagua eneo hilo la kusambaza mashuka baada ya wao kupata elimu kuwa kitanda kimoja kinahitaji mashuka 8 kwa siku ili kukamilisha mzunguko wa mgonjwa kulala katika mazingira ambayo ni safi na salama hivyo katika mipango yao ya mwaka wakaona waguse eneo hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanesco Saccos Bwana Omary Shabani ameeleza kuwa wameona ni muhimu kujikita katika Sekta ya afya ambapo wamechangia mashuka 1,300 katika Sekta nzima ya afya na kwa Mkoa wa Dodoma wametoa mashuka 300 yenye thamani ya Shilingi Milioni 23, hiyo yote ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto zinazoikabiki sekta hii ya afya.

Pamoja na kuahidi kuendelea kuifikia Mikoa mingine kwani hii ni awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza walitoa mashuka yenye thamani ya Shilingi Milioni 88 mashuka takribani 1,500 na awamu hii ya pili wameanza na mashuka 1,300.

Mashuka haya yaliyopokelewa leo na Mkuu wa Mkoa ni Mashuka 300 na  yana Thamani ya Shilingi Milioni 23 ambayo yatagwanywa katika Wilaya zote.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...