NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

LICHA ya sekta ya bahari kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa dunia, bado dunia inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mabaharia.

Ameyasema hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Salum, katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuna umuhimu wananchi kujikita katika kusoma masomo ya bahari na kupata mafunzo ya kitaalamu ili kujaza pengo lililopo la mabaharia duniani.

“Hadi sasa kuna uhaba mkubwa wa mabaharia duniani, lakini sekta ya bahari ni eneo lenye fursa nyingi, linachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa taifa na kimataifa,” amesema Bw. Salum.

Kuhusu ushiriki wa TASAC katika maonesho hayo, alisema kuwa lengo ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya fursa zilizopo katika sekta ya bahari pamoja na kujenga uelewa kuhusu kazi na majukumu ya TASAC.

Bw. Salum alibainisha kuwa TASAC ina jukumu la kusimamia masuala yote yanayohusiana na usalama wa meli, mazingira ya baharini, na utekelezaji wa Mkataba wa Usalama wa Meli na Maeneo ya Bandari (ISPS Code).

Aidha, aliongeza kuwa taasisi hiyo inahusika na ukaguzi wa vyombo vya usafiri majini, utoaji wa vibali kwa maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa bandari, pamoja na kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaotokana na shughuli za usafiri majini.

“TASAC inahakikisha vyombo vya usafiri majini vinakaguliwa mara kwa mara, usalama unazingatiwa bandarini, na mazingira ya bahari yanatunzwa kwa kudhibiti uchafuzi,” aliongeza.

Mwisho, alihimiza vijana kuchangamkia masomo ya ujuzi wa bahari na kujiunga na taasisi zinazotoa mafunzo ya mabaharia ili kujipatia ajira ndani na nje ya nchi.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...