Wafanyakazi wawili wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Mwanza TRA wamefariki papo hapo baada ya kupata ajali ya gari.
Akitoa taarifa ya ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea mnamo Julai 20 majira ya saa 10 alfajiri katika eneo la bwawani mamlaka ya mji mdogo Katoro mkoani Geita ikitokea mkoani Kagera.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni uchovu wa dereva wa gari hiyo ambayo ni mali ya TRA ambaye alikuwa ameendesha kwa muda mrefu.
Ajali hiyo inadaiwa kusababisha vifo vya watu wawili ambao ni maafisa Forodha Emmanuel Leonard na Mwita John pamoja na majeruhi mmoja Julius Dismas ambaye ni dereva wa gari hiyo ambaye alisharuhusiwa hospitali
Jeshi la polisi mkoa wa Geita linatoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za barabarani pamoja na kujipa muda wa kupumzika kabla hawajaanza safari ili kupunguza ajali za barabarani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...