CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimebuni na kutengeneza sayansi ya roketi ambayo itasaidia katika mabadiliko ya hali ya hewa.

Roketi hiyo yenye lengo yakufanya maboresho kwenye hali ya hewa.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 49 kimataifa ya sabasaba, mhadhiri mwandamizi chuo kikuu cha UDOM, Dkt. Benatus Mvile amesema Roketi hiyo itasaidia katika maboresho ya mawingu pamoja na mvua kunyesha.

“Tumeshafanya majaribio kadhaa ili kupima kwenda kwenye umbali mkubwa", amesema Dkt Mvile.

Dkt. Mvile ametaja mafanikio ya Roketi hiyo ambayo Taifa italipata ni kwenye shughuli za kilimo ikiwemo kusaidia upatikanaji wa mvua.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chuo kikuu cha UDOM, Bi. Rose Joseph, amewakaribisha wananchi katika banda la lao ili waweze kupatiwa elimu pamoja na kujionea kazi zinazofanywa na chuo hicho.

“Mwaka huu tumekuna kitofauti mwananchi anapotembelea banda letu atapata elimu juu ya lishe, na tunatoa huduma ya kisheria  bure kwa watu wote wenye uhitaji", amesema Bi. Rose Joseph.

Mwisho amesema wamejipanga kutoa elimu namna ya kujiunga na Chuo chao kwa wale wanaohitaji hufuma hiyo maana wamekuja na wataalamu.



Wananchi wakipata huduma kwenye banda la Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) leo Jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 49 kimataifa ya Sabasaba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...