Na Mwandishi wetu, Prishtina
Ujumbe kutoka Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani, Jaji Mstaafu Mhe. Awadh Bawazir umewasili Jijini Prishtina nchini Kosovo kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 14 – 18 Julai, 2025.
Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani ameambatana na Wajumbe wa Mamlaka ya Rufani, Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga, Mkurugenzi wa Mipango Wizara ya Fedha, Bw. Moses Dulle pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya PPAA.
Mwenyekiti wa Ujumbe huo, Jaji Mstaafu Mhe. Awadh Bawazir ameeleza lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kupata uzoefu wa Taasisi zinazosimamia Ununuzi wa Umma na mnyororo wa ununuzi wa umma hususan katika masuala ya ununuzi wa umma, uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroni nchini Kosovo.
Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Prishtina, ujumbe wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma ulipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kosovo Bw. Ilir Muçaj.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...