Wakati mapato ya utalii nchini yakiongezeka kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni, wadau wa sekta hiyo wamehimiza umuhimu wa kupanua wigo wa vivutio vya utalii ili kuendelea kuvutia watalii wengi zaidi kutoka duniani kote.
Wadau hao wamesema si busara kwa Tanzania kuendelea kutegemea wanyamapori na fukwe pekee kwa miaka ijayo, jambo linalochangia hata baadhi ya Watanzania kusafiri kwenda nje ya nchi kutafuta uzoefu ambao ungeweza kutengenezwa hapa nyumbani.
Akizungumza kutokea jijini Dubai siku chache baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kushinda tuzo kadhaa kubwa za World Travel Awards, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Disa Travels, Daud Lyon (@daudilyon), amesema kuna haja kubwa ya nchi kufikiria kwa upana na kuja na mbinu mpya za kukuza sekta hiyo muhimu.
“Huu ndio wakati wa kufungua fikra, kuwekeza zaidi na kubuni vivutio vipya ili Tanzania isiwe tu kivutio kwa wageni, bali pia kwa Watanzania wenyewe kutumia fedha zao hapa nyumbani,” amesema Lyon.
Amesema mfano wa kuigwa ni Dubai na Falme za Kiarabu (UAE), ambazo licha ya kutokuwa na vivutio vya asili kama Tanzania, ziliamua kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya utalii na hivyo kuifanya kuwa moja ya kitovu kikuu cha utalii duniani.
“Kadri utalii unavyokua, ndivyo unavyoinua sekta nyingine kama hoteli, usafirishaji na kuongeza ajira kwa vijana wetu. Hivyo sio jambo la kupuuzia,” amesema.
Lyon ameonya kuwa rasilimali za asili pekee hazitoshi kuleta mafanikio makubwa bila mkakati madhubuti wa kibiashara.
“Washindi wa kweli ni wale wanaoelewa soko, nani mnunuzi, nani muuzaji, na jinsi ya kuwaunganisha. Tunatakiwa tusisite kutumia fedha nyingi kwenye matangazo, maana kadri unavyowekeza kwenye kujitangaza ndivyo unavyopata fursa kubwa zaidi za kuvutia watalii,”ameongeza.
Aidha, amesema kutumia wasanii na wanamichezo maarufu kama mabalozi binafsi wa utalii ni njia rahisi na yenye mvuto wa haraka ya kuwafanya watu duniani kufikiria kuja Tanzania.
Mwisho, Lyon amepongeza Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi kufikia kutwaa tuzo hizo, lakini akasisitiza kwamba huu sio wakati wa kupumzika.
“Hongera sana kwa juhudi zenu ambazo zimeleta matokeo haya. Ila sasa ndio wakati wa kuongeza kasi zaidi na kufanya mageuzi yatakayoiweka sekta ya utalii kama injini kuu ya uchumi wetu,”amesema Lyon.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...