Wadau wa sekta binafsi mkoani Tabora wamewasilisha maoni na mapendekezo yao kwa Timu ya Kitaifa ya Wataalamu inayoratibu maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II), ambayo ipo mkoani humo kwa ajili ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali.

Timu hiyo inaendelea na  kazi ya ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau kwa lengo la kutambua mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazokwamisha biashara na uwekezaji nchini.

Lengo la zoezi hili ni kuhakikisha kuwa mchango wa sekta binafsi unazingatiwa kikamilifu katika kubaini maeneo ya kipaumbele na kuweka mikakati madhubuti ya maboresho ya sera pamoja na mazingira ya biashara na uwekezaji kwa ujumla.

Kabla ya kuanza kukutana na wadau wa sekta binafsi, Timu hiyo ilifanya kikao kifupi na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt. John Mboya pamoja na wataalamu kutoka ofisi yake na halmashauri .





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...