Na mwandishi wetu Bagamoyo

BAADHI ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wamejitokeza kutembelea vivutio vya kihistoria vilivyopo katika mji mkongwe wa Bagamoyo, wakichochewa na elimu waliyoipata kupitia banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwenye maonesho ya Sabasaba pamoja na ofa ya utalii iliyotolewa kipindi hicho.

Wakazi hao waliotembelea vivutio mbalimbali wamesema kuwa elimu waliyoipata kwenye banda hilo imewafungua macho kuhusu utalii wa ndani na umuhimu wa kuutembelea, huku baadhi wakieleza furaha yao baada ya kushuhudia kwa macho maeneo waliyoelezwa.

Agness Shayo ni miongoni mwa waliotembelea banda la TFS kwenye Maonesho ya Sabasaba na kisha kuamua kufika Bagamoyo kujionea mwenyewe vivutio hivyo.

"Nilipoelezwa kuhusu mbuyu wa ajabu ambao ukiuzunguka unaongeza siku za kuishi, nilitamani sana kuja kushuhudia. Sasa nimeona kwa macho yangu na hata kukiona kisima cha miujiza ambacho hakikauki maji," alisema Shayo kwa furaha.

Kwa upande wake, mwanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana St. Alicia iliyoko Visiga,brigiti mahanga alieleza furaha yake baada ya kufanya utalii kwa mara ya kwanza kwa njia ya mafunzo ya vitendo.

"Tunaambiwa sana kuhusu historia darasani, lakini hii ya kujionea kwa macho imeongeza uelewa wangu zaidi. Ningependa wanafunzi wengi wapate fursa kama hii," alisema na kuomba maeneo hayo yahifadhiwe vyema kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Akizungumzia hali ya wageni msimu huu, Mhifadhi wa Eneo la Kaole, Bi Siyawezi Hungo, alisema kumekuwa na ongezeko la wageni wanaotembelea vivutio vya Bagamoyo, hususan msimu wa Sabasaba, jambo linalodhihirisha mwamko wa Watanzania kuthamini urithi wa utalii wa ndani.

"Watu wanapenda kujua historia yao na sasa tunashuhudia wengi wakifika kwa ajili ya kujifunza na kushangaa urithi wa miaka zaidi ya 800 iliyopita," alisema Bi.Siyawezi

Magofu ya Kaole na Mji mkongwe wa Bagamoyo umeendelea kuwa kitovu cha historia nchini kutokana na vivutio kama Kaburi la Wapendanao, Msikiti wa wenye zaidi ya miaka 800, Mbuyu wa Ajabu na kisima cha miujiza, ambavyo vimekuwa kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi, hasa wakati wa matukio




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...