Na Hamis Dambaya, DSM.

Matangazo ya moja kwa moja kutokea hifadhi ya Ngorongoro yanayorushwa katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ndani ya viwanja vya Sabasaba jijini Dar es salaam yamekuwa kivutio kikubwa kwa watembeleaji wa maonesho hayo.

Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii akiwemo Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh.Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Utalii Dkt. Tereza Mugomi na viongozi wengine wamejionea matangazo hayo katika banda hilo.

Katika maonesho hayo wananchi wamekuwa wakijionea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Wanyamapori vilivyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kupitia matangazo ya moja kwa moja ambapo "Tv Screen" kubwa imewekwa katika banda hilo kuwezesha wananchi kufuatilia.

Akizungumzia kuhusu urushaji wa matangazo ya vivutio vya utalii kutoka Ngorongoro mpaka sabasaba Afisa Uhusiano Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro Walter Mairo amesema ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na utalii watembeleaji hupata fursa ya kuona jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia kuona vivutio wakiwa nyumbani.

“Hata baada ya sabasaba unaweza kufuatilia matangazo yetu nyumbani kupitia kurasa zetu za mitandaoni na kuona mubashara vivutio vyetu, kama unavyoona hapa spishi za Wanyamapori mbalimbali na wageni walioko hifadhi tunawaona moja kwa moja tukiwa hapa sabasaba ,”alisema Mairo.

Maonesho ya 49 ya sabasaba yanaendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ambapo Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii limekuwa kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea maonesho hayo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...