-Ashauri wawekezaji wadogo, wakati na wakubwa wote watazamwe sawa
-Asisitiza sekta ya kilimo kupewa kipaumbele kwa kinaajiri wananchi wengi
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, ameishauri serikali kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kuwa karibu na wa wawekezaji wote wakiwemo wakubwa, wa kati na wa chini ili kuongeza kazi ya kukuza uchumi.
Wasira aliyasema hayo jana alipotembelea Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba) 2025 yanayoendelea katika viwanja vya Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke Dar es Salaam.
Alisema TISEZA ni muhimu katika uchumi wa Tanzania kwa kuwa ndio inayosajili, kuwatia moyo na kuwaelekeza wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.
“Najua mnapokea wawekezaji kutoka mataifa mengine, tuanzishe utaratibu ambao utawapa motisha wawekezaji wa ndani…sekta ambayo inahitaji kuongezewa thamani ni sekta ya kilimo ambayo naamini imeajiri asilimia 65 ya Watanzania.
“Wizara ya Kilimo inafanya jitihada ya kuongeza uzalishaji, inatoa mbolea ya ruzuku kwa wakulima waweze kuzalisha zaidi lakini hiyo haitoshi, kama tukipata wawekezaji wa ndani wa kuongeza thamani ya mazao yao,” alisema.
Alisema ili kufanikiwa kiuchumi lazima wawekezaji wa ndani washawishiwe, watiwe moyo waweze kuwekeza maana wapo Watanzania wengi wanaoweza kufanya hivyo.
“Ili tutoke hapo lazima twende katika viwanda vya nguo sio lazima viwe vikubwa, ukienda India kuna viwanda vidogo vingi sana mmoja anatengeneza nyuzi na anamuuzia anayetengeneza nguo, kwa kufanya hivi tutafanya kilimo kuwa na soko la uhakika na kushusha umasikini,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...