Na Mwandishi Wetu
WAKULIMA na wadau wengine katika mnyororo mzima wa thamani wa Kilimo wameshauriwa kufanya Kilimo kibiashara ili kuongeza tija ikiwa ni kuanzia hatua za uchaguzi wa Mbegu bora na uongezaji thamani wa Mazao.
Wito huo umetolewa Leo Julai 05 na Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Filson Kagimbo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo TARI ni Miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki.
Dkt. Kagimbo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha TARI Kihinga amesema jukumu la Watafiti ni kugundua Teknolojia zinazoongeza tija kwa wadau wa Kilimo na kisha kuzisambaza ili waweze kuzitumia na ndio sababu yao kushiriki Maonesho haya wakiwa na Teknolojia mbalimbali ikiwemo bidhaa zilizoongezewa thamani anazotaja kuwa ni fursa za kijasiriliamali, biashara na kuboresha lishe za Watumiaji hususani watoto, wazee na Wajawazito.
Dkt. Kagimbo anataja Miongoni mwa bidhaa hizo kuwa ni unga lishe wa Maharage, mchicha, Mtama, Korosho.
Kwa upande wake Eliarebitha Kaaya mjasiriamali wa kuuza chakula ni moja kati ya wadau waliotembelea Banda la TARI ameeleza kunufaika kwa kujifunza kuhusu unga lishe wa mchicha unaotumika kutengeneza uji ambao anakiri kuwa ni mtamu na wenye kuboresha afya kama alivyopata elimu kwa Watafiti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...