
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Uwakala wa Meli (TASAC)limesema kuwa Sekta ya Usafirishaji kwa njia ya maji inachangia uchumi mkubwa hivyo inahitaji kulindwa na kudhibitiwa.
Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia wakati alipotembelea Banda la TASAC katika Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Nahodha Mandia amesema kuwa njia ya Usafiri wa majini kinachoangaliwa ni usalama wa vyombo pamoja na mizigo inayoingia ndani pamoja na vyombo vidogo vya ndani vinavyotumia maziwa.
Amesema kuwa katika usafiri wa bahari shehena kubwa zinazoingia ndio zinakwenda kuchochea uchumi wa nchi katika kuongeza pato la Taifa.
"Bodi tumejipanga katika kushauri katika kuona matokeo yanaonekana katika kuendelea kulinda usalama wa vyombo vya majini pamoja na abiria katika vyombo vidogo kwenye maziwa"amesema Mandia.
Nahodha Mandia amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kuwekeza katika bandari mbalimbali na miradi hiyo itakuwa na matokeo mazuri katika katika kuendelea kuchochea maendelea kwa wananchi kwa uchumi wa mtu mmoja moja hadi taifa kwa ujumla.
Amesema katika Maonesho ya yanayoendelea wananchi watembelee Banda la TASAC kupata elimu kuhusu sekta ya usafiri wa majini.
Hata hivyo amesema wananchi wanatumia vyombi vidogo katika usafiri waangalie usalama wao kwa kuwa na vifaa vya uokozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...