NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SAALM
Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Lala Lajpat Rai University of Veterinary and Animal Sciences (LUVAS) kutoka Haryana, India, wenye lengo la kukuza ushirikiano katika nyanja za elimu, utafiti, uandishi wa miradi pamoja na kubadilishana wataalamu.
Akizungumza leo Julai 11, 2025 Jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo - Utawala Prof. Amandus Muhairwa amesema kuwa makubaliano hayo yatafungua milango kwa wataalamu wa SUA kwenda India kujifunza teknolojia za kisasa pamoja na kufanya kazi kwa vitendo katika sekta ya mifugo.
"Katika makubaliano yetu tunatarajia kupeleka wakufunzi wetu kwenda kujifunza India, hasa madaktari wa mifugo ambao watapata fursa ya kufanya kazi kwenye hospitali za wanyama za LUVAS. Awamu ya kwanza nafasi zitakuwa nyingi kwa Watanzania kwenda India," amesema Prof. Muhairwa.
Aidha, amebainisha kuwa ushirikiano huo utaliwezesha SUA kujifunza teknolojia za kisasa ikiwemo uzalishaji wa mifugo kwa njia ya chupa na uhamishaji wa mimba, teknolojia ambazo zinaweza kusaidia wakulima wa Kitanzania kuboresha uzalishaji.
"Kwa sasa SUA bado hatujafikia teknolojia ya kuchagua jinsia ya ndama kabla ya kuzaliwa, lakini kwa ushirikiano huu, ndani ya miaka 4-5 tutakuwa na uwezo wa kuzalisha mbegu zinazoweza kumuwezesha mkulima kupata ndama wa jinsia anayohitaji," aliongeza.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya (LUVAS) cha Lala Lajpat Rai cha India Prof. Naresh Jindal, amesema makubaliano hayo yataimarisha uhusiano wa kitaaluma kati ya vyuo hivyo viwili, hasa katika kukabiliana na magonjwa ya mifugo kwa kutumia mbinu za kisasa.
"Ushirikiano huu utaibua fursa ya tafiti za pamoja kuhusu magonjwa ya wanyama yanayotokea katika maeneo yetu ya kikanda na kubadilishana utaalamu kwa lengo la kupata suluhisho endelevu na lenye tija kwa jamii," alisema Dkt. Jindal.
Makubaliano haya ni sehemu ya jitihada za SUA za kuimarisha ubora wa elimu ya juu na utafiti wa kisayansi kupitia ushirikiano wa kimataifa, hususan katika sekta ya kilimo na mifugo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...