Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo amepanga kukutana na wazalishaji wote wa saruji nchini hivi karubuni ili kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na wanachama wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) ambao walimwelezea changamoto zinazowakabili.
Waziri Jafo alisema wazalishaji wa saruji wameelezea kilio chao kuhusu changamoto ya umeme na upatikanaji wa gesi hivyo aliahidi kuwa mkutano huo utakaofanyika hivi karibuni utatoa majibu ya changamoto hizo.
Aliwahakikisha wenye viwanda kuwa serikali ya awamu ya sita italinda viwanda vya ndani kwa gharama zote kama mkakati mahsusi wa kulinda ajira za watanzania.
Alisema bajeti kuu ya serikali mwaka huu imeweka mazingira mazuri kuhakikisha kunakuwa na ukuaji wa kasi wa maendeleo ya viwanda hali ambayo itapunguza tatizo la ajira.
Alisema hatua ya serikali kuchukua asilimia 70 ya mapendekezo ya CTI na kuyatatua ni ushahidi dhahiri wa namna serikali ya awamu ya sita ilivyonuwia kulinda viwanda vya ndani.
“CTI mileta mapendekezo 87 na serikali imechukua 50 ambayo ni sawa na asilimia 70, huu ni ushahidi wa namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyopania kuhakikisha viwanda vya ndani vinaendelea kukua na kuzalisha ajira nyingi,” alisema
Aliwapongeza wenye viwanda kwa kuendelea kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa kuajiri vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu na kuongeza kuwa serikali peke yake isingekuwa na uwezo wa kuwaajiri.
“Mwenyekiti wa CTI, Hussein Sufian amesema hapa kwamba ajira kwenye sekta ya viwanda imeongezeka kutoka 300,000 mwaka jana hadi ajira 400,000 hii ni hatua kubwa sana kwasababu serikali haiwezi kuchukua wahitimu wote nafasi ni chache,” alisema
Aliwahakikishia wanachachama hao wa CTI kuwa Dira mpya ya 2050 imeweka kipaumbele kuendeleza maendeleo ya viwanda kwa kutambua kuwa maendeleo ya viwanda ndiyo mhimili mkuu wa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote.
Alisema kutokana na ukuaji wa viwanda nchini viwanda vya ndani vimekuwa vikizalisha bidhaa zenye ubora wa kimataifa hali ambayo imepunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Mwenyekiti wa CTI, Hussein Sufian alisema sekta ya viwanda imeendelea kufanya vizuri na imekuwa kwa asilimia 4.8 mwaka 2024/25 kulinganisha na ukuaji wa asilimia 4.3 kwa mwaka wa fedha uliopita.
Alisema CTI inafurahi kuona ajira kwenye sekta ya viwanda zinaendelea kuongezeka kufikia hadi ajira 400,000 kutoka ajira 370,000 miaka michache iliyopita.
“Haya ni maendeleo makubwa sana na hii inaonyesha ni namna gani mchango wa sekta ya viwanda kwenye ukuaji wa uchumi unaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka,” alisema
Alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa kama bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) na reli ya kisasa (SGR) ambayo inawarahishia wenye viwanda kwenye uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa.
“CTI tunafurahia sana bajeti ya serikali mwaka huu ambayo inaonyesha dhamira ya dhati ya kuendeleza viwanda na biashara na mchango wa wenye viwanda unaendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi,” alisema
Sufian alisema bajeti hiyo imeonyesha pia dhamira ya serikali kulinda viwanda vya ndani na kuongeza kuwa wenye viwanda wataendelea kushirikiana na serikali kwa kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...