-Awakumbusha kuhusu dhamana waliyobeba ya kubadili maisha ya watanzania kupitia mtaji wa shilingi Trilioni 86 waliopewa
-Afunga Kikao kazi cha Tatu cha Wenyeviti wa Bodi, Wakuu wa Taasisi
- Asema Rais, Dkt. Samia anatambua mchango wa Taasisi za umma; ana matarajio makubwa kutoka kwao
-Awakumbusha kutekeleza Maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais
-Kikao kazi chafanyika kwa mafanikio; chahusisha washiriki zaidi ya 600
Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma nchini kusimamia utekelezaji wa maazimio ya kimkakati yanayofikiwa katika vikao kazi wanavyofanya kwa kutambua kuwa wamebeba dhamana ya kuboresha maisha ya Watanzania kupitia mtaji wa shilingi Trilioni 86 ambao Serikali imewekeza kwenye Taasisi na mashirika yake.
Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 26 Agosti 2025 jijini Arusha wakati akifunga kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs FORUM 2025).
“Watanzania wanawategemea ninyi kuwabadilishia maisha, kama tunazungumza kuhusu umaskini wa watu, Serikali inapaswa kuwa kiongozi wa kuwaondolea watu umaskini wao, hivyo hamna budi kutambua kuwa mnalo deni la kuboresha hali zetu na maisha yetu.” Amesema Dkt. Biteko
Dkt. Biteko amewahakikishia Watendaji hao kuwa Serikali katika ngazi zote inatambua mchango wa taasisi na mashirika katika ukuaji wa uchumi na pia inatambua mchango wa vikao kazi vya watendaji hao ambavyo vimepelekea mashirika kuongeza mchango wake katika mfuko mkuu wa Taifa.
" Vikao kazi hivi mnavyofanya vimeonesha mchango wake katika uchumi, mfano katika kikao kazi cha mwaka 2024 mliazimia mashirika ya umma yaboreshe utendaji na kuongeza uchangiaji katika mfuko mkuu wa Serikali na matokeo yameonekana mfano Shirika la Maendeleo ya Petroli ( TPDC) liliongeza uchangiaji wake kwa asilimia 100, shirika hili liliongeza uchangiaji wake kutoka shilingi bilioni 5.5 kwa mwaka 2023/2024 hadi shilingi bilioni 11.1 mwaka 2024/2025." Amesema Dkt.Biteko
Ameongeza kuwa, uchagiaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) umeongezeka kwa asilimia 363 katika mfuko mkuu wa Serikali ambapo NHC ilichangia shilingi bilioni 1.2 mwaka 2023/ 24 na mwaka 2024/2025 ilichangia shilingi bilioni 5.5.
Dkt. Biteko amewaeleza Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi kuwa “Rais Samia pamoja na kuthamini mchango wenu kwa Serikali anatarajia mengi kutoka kwenu na Watanzania wana matarajio makubwa hasa wakati tukielekea kwenye utekelezaji wa Dira 2050, endeleeni kuongeza mchango wenu kwenye ukuaji wa uchumi, mjitegemee na muwe mfano wa taasisi binafsi."
Katika.hatua nyingine, Dkt. Biteko ametaka viongozi hao kufanyia kazi agizo lililotolewa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango la kudhibiti mianya ya uvujaji wa mapato.
Pia amempongeza Msajili wa Hazina kwa kuwa na maono ya kuratibu kikao kazi hicho ili kujadili masuala yatakayosukuma mbele utendaji wa taasisi.
Katika hafla hiyo, Dkt. Biteko hakuacha kukumbusha kuhusu ushiriki wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo
amesema uchaguzi huo uwe ni ajenda ya watu wote wakiwemo Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi hivyo waone kuwa wana wajibu wa kuwasisitiza watu kwenye taasisi zao kujitokeza kusikiliza wagombea na baadaye kupiga kura kwa amani kwani kukiwa na amani mashirika hayo pia yatafanya vizuri zaidi.
Naibu Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo kwa upande wake, amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dira na muongozo katika kuendeleza mashirika ya umma ili yaweze kuwa na tija nchini.
Amesema katika siku tatu za kikao kazi washiriki wamejifunza na kubadilishana uzoefu kupitia watoa mada wa ndani na nje ya nchi waliobobea.
Amesema Wizara ya Mipango na Uwekezaji itahakikisha maazimio ya kikao kazi hicho yanatekelezwa ipasavyo, pia Wizara itasimamia mageuzi ya kuhakikisha mashirika ya umma yanachangia ukuaji wa pato la taifa hadi kufikia Dola za Marekani trilioni 1 ifikapo 2050 ambapo kwa sasa pato la taifa ni dola za Marekani bilioni 85.
Kwa upande wake Salim Kali, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema wilaya 6 za Mkoa wa Arusha zimefikiwa na umeme hadi ngazi ya vijiji, pia miradi ya maji imefanyika pamoja na miundombinu ya Barabara ambayo imewezesha maisha bora kwa watu wa aina zote wakiwemo watalii.
Awali, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu alisema kuwa katika kikao kazi hicho kampuni zaidi 300 zimeshiriki huku washiriki wakiwa ni zaidi ya 650.
Alisema kikao kilikuwa na majadiliano mbalimbali ya kina yanayolenga kusukuma mbele uchumi wa nchi na kusimamia uwekezaji wa Serikali kwa taasisi za umma wa zaidi ya shilingi trilioni 86.
Mkutano huo wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma uliongozwa na kaulimbiu ya "Ushirikiano Endelevu wa Kibiashara katika Mazingira Shindani Kimataifa- Nafasi ya Mashirika ya Umma."

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...