Tanzania na Japan zimesaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano (MoU) katika uendelezaji wa rasilimali watu katika sekta ya ujenzi.
Uwekaji saini wa MoU hiyo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) na Naibu Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii (anayeshughulikia Miradi ya Kimataifa) wa Japan, Mheshimiwa Kenichi Ogasawara jijini Yokohama pembezoni mwa Mkutano wa TICAD9 Agosti 20, 2025
Kupitia makubaliano hayo na kwa kuzingatia teknolojia ya Japan na kampuni zake katika miundombinu bora inayodumu kwa muda mrefu na inayostahimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi, Tanzania itanufaika kuwajengea uwezo vijana wa kada za uhandisi na ujenzi kupata teknolojia na ujuzi wa Japan ili waweze kujiajiri katika kada za ujenzi na kupata ajira katika kampuni za Japan.
Makubaliano hayo yatasaidia katika kushirikisha vijana wa Tanzania na sekta binafsi katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 kupitia sekta ya miundombinu bora ambayo ni sekta mtambuka katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania.
Tanzania ni nchi ya kwanza barani Afrika kuingia makubaliano hayo na Japan katika sekta ya ujenzi, Japan imewahi kuingia makubaliano haya na baadhi ya nchi za kusini mashariki mwa Asia ambazo kupitia teknolojia bobevu ya Japan katika miundombinu bora imechagiza maendeleo ya kiuchumi ya nchi hizo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...