Na Anne Robi, Lindi

MKUU wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka Wakurungezi Watendaji na viongozi wa wilaya za mikoa ya Mtwara na Lindi kuwawezesha wakulima kufika katika viwanja vya maonesho ya nanenane Kanda ya Kusini kuangalia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo, Ufugaji na Uvuvi nchini.

Sawala ametoa maagizo hayo Agosti 1,2025 wakati akifungua Maonesho hayo ya 12 Kanda ya Kusini , 2025 katika Viwanja vya Ngongo, Mkoani Lindi.

"Nisisitize kwa Wakurugenzi na viongozi wa wilaya zote mikoa ya Lindi na Mtwara kuangalia namna ya kuwawezesha wakulima, wafugaji, na wavuvi kufika katika viwanja hivi kujionea mambo mapya, teknolojia mpya na mbinu mpya kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi," amesema.

Mkuu huyo amewataka viongozi hao kwenda maeneo mbalimbali ya wakulima, wafugaji na wavuvi kuwatangazia kuhusu maonesho ya Nanenane 2025, ili waweze kujitokeza kwenda kuangalia fursa mbalimbali kwenye sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Katika hatua nyingine, Sawala amewataka wananchi wenye sifa kujiandaa kupiga kura, kudumisha amani wakati wa kampeni na kuhamasisha pia kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wa mbungeni na kwenye Halmashauri.

Maonesho ya Nanenane 2025 yenye kaulimbiu "Tuchague Viongozi Bora kwa ajili ya Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi' yanafanyika kwa mara 32 nchini.

Maonesho hayo ni hafla ya kila mwaka inayofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 8 ikishirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali zinazohusiana na Kilimo, Mifugo,Uvuvi na Maliasili.















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...