SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema katika mageuzi ya Mashirika ya umma yanayoendelea kufanywa na Serikali, ni lazima TRC ihakikishe inafanya mabadiliko katika sekta ya biashara na ya uendeshaji kwa ushirikiano na sekta binafsi

Mkurugenzi mkuu wa TRC Mhandisi Machibya Shiwa, amebainisha hayo jijini Arusha pembezoni mwa kikao kazi cha Wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi za umma kilichoanza Agosti 23 na kufikia tamati yake Agosti 26, 2025, ambapo amesema sekta binafsi inaweza kuiwezesha TRC kupata mapato zaidi kuliko inavyojiendesha sasa.

Mhandisi Shiwa, ameishukuru serikali kwa kuruhusu sekta binafsi iweze kushiriki kwenye uendeshaji wa reli kufuatia marekebisho ya sheria nambari 10 ya reli ya mwaka 2017, yaliyofanyikwa mwaka 2023 na kusainiwa na Mheshimiwa Rais, hivyo kutoa fursa za kiuendeshaji kwa watu binafsi.

Aidha Mkurugenzi mkuu huyo wa TRC, amesema, moja ya changamoto iliyokuwa inaipata TRC ni kuwa na miundombinu mipana ambayo inatumia theluthi moja ya uwezo wake, hivyo inapoingizwa sekta binafsi inamaanisha ile sehemu ya miundombinu iliyopo TRC, sekta binafsi inaweza kushiriki na kuwezesha TRC kupata mapato zaidi kuliko inavvyojiendesha sasa.

Mabadiliko mengine amesema Mhandisi Shiwa, ni kwamba TRC inataka kuishirikisha sekta binafsi katika masuala yakiwemo ya ukarabati wa njia ya reli, vichwa na mabehewa na ikiwezekana tunakoekea TRC ibaki na jukumu la kiundeshaji tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...