#Limekuwa Mkombozi kwa wajawazito na watoto
#Kuunganisha Vijiji vya Buturu na Chifu Wanzangi
Butiama
Wananchi wa kijiji cha Buturu Wilayani Butiama Mkoani Mara wameipongeza Serikali kwa kuwajengea daraja ambalo linakuwa mkombozi kwa kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kijifungua pamoja na watoto kusombwa na maji wakati wa kwenda shule kutokana na kuwepo na bonde katika barabara kuu ya kijiji hicho.
Bw. Maningu kasombi, Mwenyekiti wa kijiji cha Buturu anasema kabla ya ujenzi wa daraja hilo la mawe wakazi wa kijiji hicho walikuwa inawalazimu kutumia gharama kubwa katika usafiri kwa kuzunguka vijiji vingine ili kufikia huduma za kijamii na ameweka wazi kuwa wajawazito asilimia kubwa walikuwa wanajifungulia njiani au majumbani kwa kukosa miundombinu mizuri ya barabara.
" Ubovu wa barabara ulikuwa unafanya akinamama kujifungulia njiani na wakati mwingine usafiri unakosekana hivyo wengi walikuwa wanajifungulia nyumbani lakini kwa sasa tunatumia barabara hii muda wowote na usafiri umekuwa wa gharama nafuu ukitofautisha na mwanzo ambapo tulikuwa tunatumia mpaka elfu 15 kufika butiama "amesema Maningu.
Licha ya changamoto hiyo ya wanawake kijifungua njiani pia Kijiji hicho kilikuwa chini kiuchumi kutokana na kushindwa kuuza mazao yao kwa wakati na kupelekea kudorora kwa mazao lakini kwa sasa wanaipongeza Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo limeleta faraja kijini hapo na kuinua uchumi wa wananchi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buturu Bi. Grace Richard anaipongeza Serikali kwa ujenzi wa daraja hilo ambalo limeenda kuongeza maudhurio ya wanafunzi shuleni hapo tofauti na awali ambapo ilikuwa inawalazimu Wazazi na Waalimu kuwavusha watoto katika bonde hilo ili waweze kwenda shule kutokana na bonde hilo kuwa na maji mengi hali ambayo ilikuwa ikichangia utoro shuleni.
"Ilikuwa ikifika kipindi cha masika shule yetu ilikuwa na changamoto ya utoro kutokana na watoto wengi kushindwa kuvuka kwenye bonde na kuja shule ukizingatia wanafunzi wengi wapo upande wa pili na ilikuwa inatulazimu waalimu na wazazi kuwavusha watoto ili waweze kufika shule hii ilikuwa inaathiri wakati mwingine ufundishaji"
Awali akisoma Taarifa ya mradi wa ujenzi wa Daraja la mawe Meneja wa Tarura Wilaya ya Butiama Mhandisi Rashidi Kavandama amesema mradi huo umegaharimu kiasi cha Shilingi Milioni 299.26 na daraja lina ulefu wa Mita 32 na upana wa Mita 7.7 ambapo daraja hili ni sehemu ya Miradi ya maendeleo inayojengwa na Serikali ya awamu ya sita kupitia fedha za mfuko wa bodi ya Barabara.
Mhandisi Kavandama ameongeza kuwa ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa 100% na kukamilika kwa mradi huo kumesaidia wananchi kuzifikia huduma za kijamii kwa urahisi kama huduma za kiuchumi na kijamii kama vile Afya, Elimu na Biashara.
Aidha, Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi amezindua daraja hilo ambalo limekuwa kiungo muhimu kwa wakazi wa kijiji cha Buturu na Chifu Wanzangi na kusema daraja hilo limeleta matumaini kwa Wananchi wa eneo hilo .
" Ombi langu kwa wananchi wa eneo hili nitumie fursa hii kuwaasa mtunze miundombinu hii ya daraja ili iweze kuwa imara zaidi na kutumika kwa muda mrefu zaidi"
Ussi pia ameipongeza Tarura kwa kutumia mawe kujenga daraja hilo kwani kumeweza kupunguza gharama za ujenzi kwa kiasi kikubwa tofauti kama wangeamua kulijenga kwa kutumia zege.
" Nawapongeza ofisi ya Tarura Mkoa wa Mara na Wilaya ya Butiama kwa kuwa wazalendo kwelikweli wameamua kujenga Daraja hili kwa kutumia mawe na limegharimu Fedha isiyozidi milioni 500 hili ni jambo la kuwapongeza kweli kwa uzalendo wao".

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...