-Miradi ya zaidi ya Shilingi Milioni 160 yatekelezwa.
-Utoro wapungua; Ufaulu waimarika
Na Mwandishi Wetu – Uyui
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wameendeleza juhudi kubwa za kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi Wilayani Uyui, mkoani Tabora, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuinua ubora wa elimu nchini.
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano maalum yaliyosainiwa kati ya TEA na UNICEF, yenye lengo la kuboresha miundombinu ya elimu katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Songwe. Kupitia ushirikiano huo, jumla ya miradi 48 ya elimu inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, miradi minne tayari imekamilika, ikiwa na thamani ya takriban shilingi milioni 162.8. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Nsololo, pamoja na ukarabati na umaliziaji wa maabara nne za masomo ya sayansi katika shule za sekondari za Goweko, Usagari na Kizengi.
Utekelezaji wa miradi hiyo umekuwa chachu ya maboresho makubwa katika mazingira ya kujifunzia, na hivyo kuchochea ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi mmoja mmoja pamoja na maendeleo ya kitaaluma katika shule kwa ujumla.
Mazingira bora, ufaulu waimarika
Mkuu wa Shule ya Sekondari Nsololo, Mwalimu Paulina Mereka, alisema kabla ya utekelezaji wa mradi huo, shule ilikuwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya vyoo.
"Shule yetu ina wanafunzi 500 lakini tulikuwa na matundu manne tu ya vyoo, yaliyotumiwa na wanafunzi na walimu. Hali hii ilikuwa changamoto hasa kwa wanafunzi wa kike, na kwa kweli iliathiri mahudhurio na utulivu wa ujifunzaji," alisema Mwl. Mereka.
Aliongeza kuwa, ujenzi wa matundu 10 ya vyoo umekuwa mkombozi mkubwa kwa shule hiyo na umeleta matumaini mapya katika ukuaji wa taaluma.
"Sasa tuna uhakika wa ongezeko la mahudhurio, mazingira salama ya kujifunzia, na pia ufundishaji utaimarika. Tunaamini hali hii itaongeza ufaulu wa kitaaluma shuleni," alisisitiza.
TEA na UNICEF wanaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ya elimu ili kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya kujifunza katika mazingira bora, salama na rafiki kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kusimamia upatikanaji wa elimu bora na kwa usawa kote nchini.

Muonekano wa nje wa maabara ya Sayansi Shule ya Sekondari Goweko iliyopo Wilayani Uyui, Mkoani Tabora.
Muonekano wa ndani wa maabara ya Sayansi Shule ya Sekondari Goweko iliyopo Wilayani Uyui, Mkoani Tabora
Kaimu Meneja Miradi ya Elimu kutoka TEA Bi. Mwafatma Mohamed (Katikati) akiongea na walimu wa Shule ya Sekondari Goweko mara baada ya kukagua maabara iliyofadhiliwa na UNICEF kwa usimamizi wa TEA shuleni hapo.
Muonekano wa ndani wa choo cha kisasa kilichojengwa shule ya Sekondari Nsololo Wilayani Uyui, Mkoani Tabora
Muonekano wa vyoo bora na vya kisasa shule ya Sekondari Nsololo Wilayani Uyui, Mkoani Tabora
Muonekano wa nje wa vyoo vilivyojengwa kwa ufadhili wa UNICEF na kusimamiwa na TEA katika shule ya Sekondari Nsololo Wilayani Uyui, Mkoani Tabora
Maandalizi ya kubandika kibao kuonesha ukamilikaji wa mradi yakiendelea shule ya Sekondari Nsololo
Muonekano wa nje wa maabara mbili za Sayansi shule ya Sekondari Usagari, iliyopo Wilayani Uyui, Mkoani Tabora

Muonekano wa kibao cha kukamilika kwa mradi katika shule ya Sekondari Goweko

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...