Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua Kampeni ya Elimu ya Kodi kwa Biashara za Mtandaoni kwa lengo la kuhakikisha kila anayehusika na biashara hizo anajisajili ili aanze kulipa Kodi.

Akizindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam Kamishna Mkuu wa TRA ,Yusuph Mwenda amesema wanaolengwa katika usajili huo ni Wafanyabiashara wenye kipato cha zaidi ya Sh. Milioni 4 kwa mwaka ambao Kodi yao itakuwa Sh. 100,000 kwa mwaka na kila mmoja atalipa kulingana na kipato chake.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema wakati wakiendelea kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara wote wanaofanya biashara za mtandaoni kujisajili, wataanza na wanaofanya biashara ya kukodisha nyumba mtandaoni pamoja na wale wanaoendesha biashara mtao ambao wamekuwa wakipata fedha nyingi na hawalipi Kodi.

Amesema TRA itatoa asilimia 3 ya Kodi itakayookolewa kwa watu watakaotoa taarifa za ukwepaji wa Kodi kwa Wafanyabiashara watakaoshindwa kujisajili ndani ya muda uliowekwa na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wanaokwepa Kodi na watawatambua kwa kutokutoa risiti.

"Kila anayestahili kulipa Kodi atalipa kulingana na uwezo wake na mtaji wake na tupo kwaajili ya kuwezesha biashara hivyo hakuna mtu atakayeonewa katika utozaji wa Kodi" amesema Mwenda.

Amesema ili kuwezesha biashara wanaanzisha kitengo cha kuwezesha biashara katika kila mkoa wa Kodi kitakachosaidia kurahisisha ufanyaji wa biashara na kutatua changamoto za Walipakodi ili kuwawezesha kulipa Kodi kwa hiari.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema ili kuhamasisha matumizi ya mtandaoni TRA imepunguza viwango vya VAT kutoka asilimia 18 mpaka 16 kwa Walipakodi watakaofanya malipo kupitia Mtandaoni na utekelezaji wa jambo hilo utaanza September Mosi mwaka huu.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana amesema hivi sasa mifumo ya BASATA inasomana na mifumo ya TRA Hali ambayo imerahisisha utoaji huduma na usajili wa wasanii na kazi za Sanaa na kurahisisha ulipaji wa Kodi kwa hiari.

Mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. John Daffa amesema wao ndiyo wasajili wa mitandaoni yote na Kampuni zinaxoendesha shughuli za Mawasiliano nchini hivyo watashirikiana na TRA kuhakikisha ulipaji Kodi kwa Biashara za Mtandaoni unafanikiwa.

Amesema kila mtanzania anapaswa kuona fahari kulipa Kodi kwa hiari ili kuchangia maendeleo ya Taifa.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...