-Asisitiza kuendelea kusimamiwa kwa Itifaki ya SADC dhidi ya Rushwa.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa wa Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kusimamia kikamilifu na kwa ufanisi utekelezaji wa Itifaki ya Jumuiya hiyo dhidi ya Rushwa ili kujenga ukanda usio na Rushwa.
Amesema kuwa Itifaki ya SADC Dhidi ya Rushwa bado ni nyenzo muhimu katika kufanikisha utawala bora, amani na muungano endelevu wa kikanda hivyo viongozi hao wanapaswa kuhakikisha kuwa juhudi za kupambana na rushwa zinaendelezwa.
Ametoa wito huo leo (Agosti 04, 2025) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Ufunguzi wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Utekelezaji wa Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Dhidi ya Rushwa, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.
“Lazima tukiri kwamba rushwa ni tishio kwa usalama. Inachochea uhalifu uliopangwa, usafirishaji haramu wa binadamu, ugaidi, na kudhoofika kwa utawala wa sheria.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni, nchi Wanachama wa SADC ikiwemo Tanzania zimeendelea kuimarisha sheria za mapambano dhidi ya rushwa, kuziwezesha Taasisi zinazosimamia udhibiti na mapambano dhidi ya rushwa pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za rushwa kwa ustawi wa Taifa.
“Hata ushirikiano wa kikanda katika mapambano dhidi ya rushwa umeimarika kwa kubadilishana taarifa, mashirikiano katika masuala ya sheria pamoja na uchunguzi wa pamoja katika kushughulikia masuala ya rushwa ya kikanda”
Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania kwa upande wake, inachukulia mapambano dhidi ya rushwa kama kipaumbele cha kitaifa na jambo la msingi kwa maendeleo Taifa na usalama wa Taifa.
“Njia iliyo mbele huenda ikawa ndefu, lakini tusiwaze kushindwa. Kwa ushirikiano endelevu, maono ya kimkakati, na utashi wa kisiasa, tunaweza na tunapaswa kujenga ukanda wa SADC usio na rushwa”
Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza viongozi hao kwa kuendelea kusimamia mikakati mbalimbali ya kupiga vita rushwa ikiwemo kuanzishwa kwa mfumo imara ya ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa SADC. Pamoja na Kielelezo cha Jitihada za Kikanda za Kupambana na Rushwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stegomena Tax amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kusimama imara katika kuendeleza utawala bora na kuheshimu utawala wa sheria, ambayo ni nguzo kuu katika mapambano yao ya pamoja dhidi ya rushwa.
“Warsha hii, imekuja wakati muafaka, ikiwa ni jukwaa la kubadilishana uzoefu bora, kuimarisha ushirikiano, na kuoanisha juhudi zetu katika kupambana na rushwa kwa ufanisi zaidi katika ukanda huu.”
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kupambana na Rushwa ya SADC, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila amesema kuwa kupitia mikakati Miwili ya Kupambana na Rushwa ya (2018-2022) na (2023-2027), wamefanikiwa kuandaa mtaala wa Kikanda uliowekwa viwango vya uchunguzi na kinga dhidi ya rushwa, kuandaa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Kikanda wa Kupambana na Rushwa pamoja na Kuandaliwa kwa Tathmini ya Kikanda ya Mapambano Dhidi ya Rushwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...