Pwani, Septemba 24, 2025 – Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariam Ibrahim, ameungana na Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Pwani katika maandalizi ya kumkaribisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mariam ametembelea maeneo mbalimbali ya mkoa huo akihamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kumpokea Rais Samia, huku akitoa pongezi kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa chini ya uongozi wake.


“Namshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia kwa mambo makubwa aliyoyafanya Mkoa wa Pwani. Kupitia uongozi wake tumepata fedha za kukamilisha miradi ya maji, shule za sekondari na msingi, hospitali, vituo vya afya, zahanati, pamoja na kupeleka umeme katika kila kijiji. Pia tumeshuhudia upanuzi wa barabara kutoka Mbagala Rangitatu hadi Mkuranga baada ya kupata kibali kutoka kwake,” alisema Mariam.


Aidha, Mariam alisisitiza kuwa wananchi wa Pwani wanathamini jitihada hizo na hawana cha kumlipa Rais Samia zaidi ya kumpa kura nyingi za kishindo katika chaguzi , ili aendelee kuwaletea maendeleo.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...