Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule ameitaka jamii na wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana kwa kuwekeza katika sekta ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo ili kuwasaidia vijana ambao hawakufikiwa na programu za serikali waweze kunufaika.


Ametoa wito huo Septemba 04,2025 wakati alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert John Chalamila katika maadhimisho ya Juma la Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo Rasmi 2025, yaliyofanyika katika uwanja wa CCM Mwinjuma , Mwananyamala jijini Dar es Salaamambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema "kukuza kisomo katika zama za kidigitali kwa maendeleo endelevu ya taifala Tanzania. "

Pia DC Mtambule ameitaka jamii kuendelea kushirikiana katika kupambana na vikwazo vinavyowafanya vijana hasa wa like washindwe kufikia  ndoto zao kutokana na mmomonyoko wa maadili na ukatili wa aina yeyote ile kwani kila mtu anajukumu la kupaza sauti ili kutoa fursa kwa vijana kuweza kupata haki yao ya kisheria ya elimu kwaajili ya kujikwamua katika wimbi la umasikini.

Amesema kuwa  vijana 3,570 waliokuwa nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa mwaka 2023-2025 wamenufaika kupitia mpango wa kuwawezesha vijana wa kitanzania ambao kutokana na umasikini na ukatili wanaofanyiwa hasa kwa watoto wakike walishindwa kufikia ndoto zao.

Pamoja na hayo DC Mtambule amewataka wananchi wajitokeze katika zoezi la uchaguzi mkuu oktoba 29,2025 kwa kuwachagua viongozi bora watakaoendelea kuimarisha amani na utulivu wa nchi kwani hiyo ni fursa ya kikatiba na sheria kushiriki katika uchaguzi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...