Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Bahi

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Ujenzi wa kituo cha treni ya mwendo kasi (SGR) pamoja na bandari kavu zinazokwenda kujengwa Wilaya ya Bahi inakwenda kuvutia uwekezaji na kufungua fursa za ajira kwa vijana.

Akihutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Dk.Samia aliyesimama kuomba kura kuelekea Uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu ,amesema kuna ujenzi wa SGR ambako pia kutakuwa kituo cha treni hiyo katika awamu ya pili na ya tatu ya ujenzi.

“Pia patakuwa na kituo na bandari kavu ambayo inakwenda kuibadilisha Bahi kwa sababu kituo cha SGR na bandari kavu inakwenda kuvutia uwekezaji, biashara na kwamaana hiyo ajira zitakuwa nyingi kwa vijana wetu.Bahi inakwenda kufunguka.”

Aidha, kwa upande mwengine amesema anatambua kuna madai ya fidia kwa waliopisha mradi wa reli ya SGR lakini na miradi mingine hivyo ameahidi madai hayo wanayafanyia uhakiki na wakapomaliza fidia zinakwenda kulipwa.

Kuhusu barabara amesema kipindi cha miaka mitano ujenzi wa miradi ya barabara na miundombinu ya barabara itaendelea.”Tumejitahidi kwenye barabara na miundombimu ya barabara…

“Kwani hapa Bahi tumejenga madaraja 9 na barabara za changarawe kilometa 152 ambapo sasa zinapitika muda wote.”Lakini nafahamu bado kuna uhitaji wa barabara kwa kiwango cha changarawe.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...