Na Said Mwishehe,Michuzi TV- Pwani
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan mipango ya Serikali katika mitano no ijayo inatarajia kujenga njia sita za magari na njia mbili za mwendokasi kuanzia Mailimoja hadi Picha ya Ndege katika barabara ya Morogoro mkoani Pwani.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni leo Septemba 28,2015 katika mkutano wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu ,Dk.Samia amesema anatambua mahitaji ya miundombinu hiyo kwa sababu ya msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro kutokana na wembamba wa barabara hiyo.
Amesema kwamba tayari usanifu unaendelea kwa upanuzi wa barabara kutoka Mailimoja hadi Picha ya ndege ili iwe na njia sita za magari na njia mbili za mwendokasi.
Vilevile, amesema serikali itaboresha mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 71, pia uboreshaji barabara kilometa 17 katika mji huo.
“Kwa kushirikisha sekta binafsi kupitia ubia na serikali, utatekelezwa ujenzi wa barabara ya haraka kutoka Kibaha - Chalinze - Morogoro itakayojengwa kwa awamu.”
Dk.Samia amesema kuwa barabara hiyo inatija kubwa kiuchumi, hivyo kupitia njia ya PPP ili fedha za serikali ziende katika miradi mingine ya huduma za jamii.
Akieleza zaidi amesema pia Serikali itajenga barabara ya Bagamoyo - Mlandizi -Manelomango yenye urefu wa kilometa 100 kwa awamu ya kwanza tumeshaingia makubaliano na mkandarasi kujenga kilometa 23 kuanzia Mlandizi hadi stesheni ya SGR Ruvu.
"Tumeanza ujenzi pia wa barabara ya TAMCO Kibaha hadi Mapinga Bagamoyo ambayo kilometa zote 23 zipo katika hatua mbalimbali za ujenzi na mwakani tutakamilisha ujenzi huu," amesema.
Ameongeza kuwa serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Utete - Nyamwage ambazo zitazidi kufungua mkoa huo.
Pia ameahidi katika miaka mitano ijayo pia serikali itakamilisha barabara ya Dar es Salaam - Kibiti - Mingoyo yenye urefu wa kilometa 487.
Kuhusu biashara,Dk.Samia amesema katika jitihada za kuboresha mazingira ya biashara kwa wafanyabiashara na wawekezaji, serikali itajenga soko la kisasa eneo la Lolindo kwa gharama ya sh. bilioni 18.
"Tutandeleza ujenzi wa stendi Kibaha vijijini lakini tutaangalia uwezekano wa stendi ya kusini.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...