-Awapongeza watumishi sekta ya umma na binafsi kwa kusimamia matumizi vizuri
-Maombi ya Hussen Bashe aahidi kwenda kufanyia kazi limo Nzega iwe mkoa
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Nzega
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambao unafanyika nchini kwa kutumia fedha nyingi inayokusanywa kwasababu wamesimamia matumizi vizuri.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora katika mkutano wa kuomba kura kuelekea Oktoba 29,2025 Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza watumishi wa sekta ya umma na binafsi kwa kusimamia vema utekelezaji wa maendeleo nchini.
“Niseme moja kubwa ambalo sijalisema kokote, kazi zote hizi za maendeleo tutazozizungumza hapa zimetumia fedha nyingi sana inayokusanywa ndani. tunayokopa nje na ile tunayopewa na marafiki.
“Lakini miradi imewezekana kujenga Tanzania nzima na kila unaposimama hadithi ni nyingi tumeleta maji, tumeleta umeme, umeleta kilimo, afya. Lakini imewezekana kwa sababu tumesimamia matumizi mazuri ya fedha.Tumesimamia matumizi mazuri na watumishi wetu, tumeweza kuwaweka kwenye mstari wa kusimamia matumizi, pia kuepuka rushwa.”
Dk.Samia amesema fedha hizo wangeacha mianya ya rushwa ,wasingesimamia vizuri fedha hizo miradi inayozungunzwa leo isingekuwepo kwa hiyo Watanzania kwa upande mwingine tumefanyakazi kubwa kupunguza rushwa.
“Na hata tafiti zinazofanywa na mashirika ya kimataifa kila mwaka Tanzania inapanda juu katika viwango vya kupunguza rushwa ndani ya nchi.Kwa pamoja tuwapongeze watumishi wa serikali hata watumishi waliopo sekta binafsi na wenyewe wanafanyakazi kwa viwango.
“Kwa hiyo tuwapongeze sana watumishi wetu kwani wamesimamia vyema kupunguza viwango vya rushwa na ndiyo maana maendeleo yanaonekana. Nchi zilizotawaliwa na rushwa hawazungumzi tunayoyazungumza leo sisi ndugu zangu Tanzania yetu tujipongeze sana,”amesema Dk.Samia.
Pamoja na hayo Mgombea Urais Dk.Samia pia ametoa ahadi iwapo wananchi watakipa ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Serikali itajenga machinjio manne na majosho sita wilayani Nzega.
Pia ameahidi Serikali itaendelea kutoa ruzuku ya chanjo kwa mifugo, hivyo amewaomba wafugaji kupeleka mifugo yao kwenye chanjo.”Pia itambulike ili Tanzania iingie kwenye ramani ya kimataifa kwenye masuala ya ufugaji.”
Kuhusu maji,Dk.Samia Serikali katika miaka mitano ijayo itaendelea kuimarisha upatikanaji maji wilayani Nzega ambapo kutakuwa na awamu ya pili ya mradi wa Ziwa Viktoria.Kupitia mradi huo maji yatapelekwa kata za Bukene, Mwamala, Itobo, Isanzu, Kasela, Buduka, Shinyanga na Itindwa.
Dk.Samia ameeleza lengo ni kuwasaidia wananchi 85,607 katika kata hizo ambao wanaokwenda kufaidika na mradi huo pindi wakipata ridhaa.
Kuhusu miundombinu ya barabara, Dk.Samia ameahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo ikiwemo barabara ya Nzega - Itobo - Kagongwa yenye urefu wa kilometa 65 ambapo serikali imejipanga kutekeleza na kukamilisha mradi huo.
Akizungumzia maombi yaliyotolewa na mgombea ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Husesein Bashe ya kuomba Nzega iwe Mkoa, Halmashauri ya Bukene na Halmashauri ya Nzega pamoja na ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujengwa Nzega, Rais Dk.Samia amesema amepokea maombi hayo na Serikali itakwenda kuyafanyia kazi.
“Maombi yote matatu yaliyowasilishwa nimeyachukua kwenda kuyafanyiakazi.Mwenyewe anajua ndiyo maana kaniambia usinijibu hapa lakini yabebe ukayafanyie kazi.
“Kwahiyo kuna halmashauri, kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujengwa Nzega na hili na mkoa tutakwenda kuyafanyiakazi. Tutakwenda kuyafanyia kazi na majibu ni mawili tu inawezekana au haliwezekani. Lakini tunakwenda kuyafanyiakazi.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...