Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Septemba 22, 2025 ametembelea Halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika Jimbo la Iringa Mjini na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo jimbo la Kilolo Mkoani Iringa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya majimbo hayo kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.

Jaji Mwambegele pia alipata fursa ya kushuhudia Kampeni za Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Makini (MAKINI), Mhe. Coster Jimmy Kibonde na Mgombea Mwenza, Mhe. Aziza Haji Suleiman waliokuwa katika Mkutano wa Kampeni Stendi ya Zamani ya Mkoa wa Iringa majira ya Saa 10 jioni.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia taa zitakazotumika wakati wa kuhesabu kura endapo giza litaingia na hakuna umeme katika kituo ambazo zimehifadhiwa katika ghala la Manispaa ya Iringa.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia masanduku ya kura katika ghala la Manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia masanduku ya kura katika ghala la Halamshauri ya Wilaya ya Kilolo.



Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akiangalia vifaa vya Uchaguzi katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.


Watendaji hao wa Uchaguzi kutoka Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume.


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.





Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Kilolo Mkoani Iringa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...