Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mtwara
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hasssn amesema mpango Serikali katika miaka mitano ijayo ni kwenda kuongeza maeneo yaliyotengwa, kupimwa na kisha kumilikishwa kwa wafugaji kutoka ekari milioni 3.4 hadi kufikia milioni sita.
Akizungumza leo Septemba 23,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Serikali inakwenda kuongeza eneo la ufugaji ambako katika utekelezaji huo utafanyika mpaka mwaka 2030.
“Utekelezaji huo ni hadi kufikia mwaka 2030 lengo ni kuondoa changamoto ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji.Tunakwenda kuwapimia maeneo wafugaji wabaki maeneo yao na wakulima wabaki wakifanya shughuli zao.Tunataka kumaliza kabisa migogoro katı ya wakulima na wafugaji.”amesema Dk.Samia.
Wakati anaelezea mpango huo wa Serikali Dk.Samia alisema zamanı katika eneo la Nanyumbu na Mtwara kwa ujumla hakukua na ng’ombe kama ilivyo hivi sasa,ng’ombe wamekuwa wengi lakini mpango wetu Serikali ni kwenda kuongeza maeneo ya wafugaji ili wafuge katika eneo lao na wakulima waendelee na shughuli za kilimo.
Kuhusu kilimo,Dk.Samia alipokuwa anahutubia maelfu ya wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumuona na kumsikiliza amesema anawapongeza wananchi kwa kutumia vizuri mbolea na pembejeo za ruzuku zinazotolewa na serikali.
"Zimeweza kuongeza mazao kwamba korosho zimetoka tani 15,000 hadi tani 24,000 hii korosho mara ya mwisho imeingiza ndani ya Nanyumbu sh. bilioni 73 ambazo zipo mikononi mwa wakulima,"amesema.
Pia amesema katika uzalishaji karanga umepanda kutoka tani 26,100 zenye thamani ya sh. bilioni 65 hadi tani 33,170 zenye thamani ya sh. bilioni 82.9.
“Katika ufuta uzalishaji umeongezeka kutoka tani 1,580 hadi zenye thamani ya sh. bilioni 3.9 na kuvuka malengo ya kuzalisha tani 11,800 zenye thamani ya bilioni 38.8.”
Kwa upande wa mbaazi amesema zao hilo zamani lilikuwa likitumika kama mboga lakini sasa ni zao la biashara."Tumeongeza uzalishaji wa tani 1,130 ambazo zilikuwa na thamani ya sh. bilioni moja hadi tani 5,950 zenye thamani ya sh. bilioni 10.8 ambazo zimeingia kwa wakulima.
"Tukisikia kazi na utu tunasonga mbele, kazi hii ya kuleta pembejeo na mbolea kukuza kilimo ili wakulima wapate fedha iliyoingia mikononi mwao ni kuujenga utu wao.Fedha hizo zitawawezesha wakulima kujenga makazi bora, kusomesha watoto, kupata matibabu na kuimarisha uchumi wao.
Mgombea Dk.Samia amesema manufaa hayo ni kutokana na ruzuku zinazotolewa pia amewahakikishia wakulima kuwa serikali inakwenda kukamilisha ujenzi wa skimu za umwagiliaji za Likokona, Lukula na Masuguru.
Akieleza zaidi amesema Serikali itaendelea kutafuta masoko zaidi kwa kuwa bidhaa hizo ni biashara zenye misimu ya kupanda na kushuka kwa bei."Serikali yenu tunaendelea kutafuta masoko zaidi ili kulinda bei za mazao ambayo kiuhalisia hutegemea soko la kimataifa.
"Tunakwenda tupo katika mazungumzo na hatupo katika hatua mbaya kwani bei hazitoshuka kama vile ambavyo watu wanasema”
Pamoja na hayo amesema katika kuhakikisha mazao ya wakulima yanauzwa kwa bei ya uhakika, serikali itaanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao.
Amesisitiza kwamba kongani za viwanda zitawekwa katika maeneo mbalimbali badala ya kuuza malighafi tuuze mazao ambayo yameshaongezewa thamani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...