Na Mwandishi Wetu- Karatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini na kujua kazi na mchango wa waongoza watalii nchini Tanzania.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi ameyasema hayo katika tukio la Fainali ya Safari Field Challenge Toleo la 10, likiambatana na maadhimisho ya Miaka 10 ya mashindano haya, sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani lililofanyika kwenye ukumbi wa Oasis Wilayani Karatu, Arusha usiku wa Septemba 27,2025.

“Rais Samia anafahamu tunafanya tuzo hapa leo na ameangalia challenge zote mlizofanya na amekubali na akasema anawapenda sana na anawaelewa sana na ndio maana alifanya filamu ya Tanzania the Royal Tour, alikwenda Pemba akavua Samaki” amesema Dkt. Abbasi.

Aidha, Dkt. Abbasi ametumia fursa hiyo kuwahimiza waongoza watalii kushiriki katika tuzo za utalii na uhifadhi zinazotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025.

“Tumezindua tuzo za utalii na uhifadhi, ni tuzo za ushindani watu watashindanishwa kwenye kategoria mbalimbali hivyo mshiriki katika kupambania kategoria mbalimbali ikiwemo ya safari guide, mountain guide n.k” amesema Dkt. Abbasi.

Amesema kuanzi tarehe 10 mwezi Oktoba tuzo zitafunguliwa na zitakuwa na kategoria saba zenye tuzo zaidi ya 56, na tarehe 19 itakuwa ni usiku wa tuzo.




Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...