Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa Taifa Group Limited ("Taifa Group") tunapenda kukanusha kwa dhati na kwa uwazi tuhuma zisizokuwa na msingi zilizotolewa hivi karibuni kuhusu miamala iliyofanywa na kampuni zetu tanzu za Tancoal Energy Limited (TANCOAL) na Williamson Diamonds Limited (WDL) Tuhuma hizo zinahusu ununuzi wa hisa katika Tancoal na WDL. 


Madai hayo hayana msingi wowote na ni upotoshaji mkubwa wa miamala ambayo ilifanywa kwa kuzingatia sheria za nchi yetu na za kimataifa kwa kuzingatia uwazi.

MUAMALA WA TANCOAL

Mnamo mwezi Novemba 2021, kampuni yetu tanzu iliingia makubaliano ya kununua hisa zote za Intra Energy Corporation Ltd ("IEC") katika Intra Energy (Tanzania) Limited (IETL), kampuni ambayo inamilikiwa kwa asilimia mia moja na IEC. Baada ya muamala huo, sasa IETL inamilikiwa na Taifa Group, kupitia kampuni yetu tanzu ya Mirambo Mining Limited. 


IETL ndio mbia katika kampuni ya TANCOAL pamoja na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Muamala huu ulihusisha uuzwaji wa hisa na madeni yote ya kampuni ya IEC. Aidha, umiliki na hisa za moja kwa moja ndani ya kampuni ya TANCOAL, hazijawahi kubadilika tangu kampuni hiyo isajiliwe. Muamala huu ulitangazwa rasmi hadharani tarehe 25 Novemba 2021 kwa mujibu wa kanuni za soko la hisa la Australia (ASX.) Ni muhimu umma ufahamu kwamba IEC imesajiliwa kwenye Soko la Hisa la Australia (ASX: IEC).


MUAMALA WA WDL

Aidha, mwezi Januari 2025, kampuni yetu tanzu lilinunua hisa zote pamoja na madeni ya Petra Diamonds Limited ("Petra") katika WDL. Ni muhimu umma ufahamu kwamba Petra imesajiliwa kwenye Soko la Hisa la London (LSE: PDL). Muamala huu ulitangazwa rasmi tarehe 22 Januari 2025 kwa mujibu wa masharti ya udhibiti ya soko hili nchini Uingereza.


Katika matukio haya yote mawili, hisa ziliuzwa na kampuni zilizoorodheshwa kwenye masoko ya kimataifa ya hisa, na siyo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Madai yanayosema vinginevyo si ya kweli kwani sio tu hayana ushahidi wowote, bali pia yana nia mbaya ya kuzua taharuki.


NB: Soma Swipe picha zilizowekwa kusoma zaidi

                 https://www.instagram.com/p/DOX_03oguMM/?igsh=MWtkbmg1ajZzcWR2Yg==

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...