Na Pamela Mollel,Manyara
Shule ya Tarangire Pre & Primary English Medium School (Tarangire School) imeibua ubunifu wa aina yake baada ya kufanya mahafali ya darasa la saba kwa mwaka 2025 ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, tukio ambalo halijawahi kushuhudiwa mkoani Manyara.
Mahafali hayo yaliyofanyika Jumamosi, Septemba 13, 2025, yaliwaaga wanafunzi 40 walioketi mtihani wa kitaifa wa darasa la saba Septemba 10 na 11, 2025. Sherehe hizo zilihudhuriwa na walimu, wafanyakazi wa shule, wazazi na wanafunzi waliobaki, na kuacha alama ya kipekee kwa mji wa Babati na mkoa mzima.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkuu wa Shule, Ndugu Amos Temu, alisema dhumuni kuu la Tarangire School ni kutoa elimu yenye thamani endelevu (Sustainable Value) kwa wadau wake wote.
Kwa upande wake, mmoja wa wahitimu, Joan Wilberd Njau, aliushukuru uongozi wa shule kwa kuanzia na Meneja, Bi Flora Ronald, pamoja na walimu na wafanyakazi wote, akisema wamechangia kwa kiasi kikubwa kuinua elimu mjini Babati na Manyara kwa ujumla.
Ubunifu huu wa kufanyia mahafali hifadhini umeonesha dira ya shule hiyo katika kuhamasisha wanafunzi si tu kwenye masomo, bali pia katika kuthamini mazingira, utalii na urithi wa taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...