GEITA

Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Geita Bi. Eva Ikula amewatakawafanyabiashara wa madini mkoani humo kuzingatia matumizi ya vipimo sahihikatika biashara yao ili kuhakikisha kunakuwa na usawa kwa pande zotezinazohusika na kuepusha upande wowote kupunjika.

Ametoa wito huo Septemba 25, 2025 alipozungumza na waandishi wa habarikatika maonesho ya kimataifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika katikaviwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mjini Geita, yenye kaulimbiu “ukuaji wasekta ya madini ni matokeo ya matumizi ya teknolojia sahihi na uongozi bora, shiriki uchaguzi mkuu oktoba 2025”.

Ikula ameeleza kuwa, WMA ina mchango mkubwa katika sekta ya madini ambapobiashara hiyo haiwezi kufanyika pasipo kuwa na mizani iliyohakikiwa nainayotumika kwa usahihi ili kuhakikisha kunakuwa na usawa baina ya pande mbilizinazofanya biashara.

Kadhalika, amesema kuwa, katika sekta ya madini, mojawapo ya majukumu yaWMA ni kuhakikisha mizani zote zinazotumika kuuzia na kununulia vito namadini zinahakikiwa na zinapima madini kwa usahihi.

Ameongeza kuwa, Wakala pia hutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na mizanizinazopaswa kutumika kuuzia madini kwa kuwa siyo mizani zote zinastahilikutumika kuuzia na kununulia madini.

“Katika mwaka wa fedha 2025/2026, Mkoa wa Geita unatarajia kuhakiki mizani197 zinazotumika katika sekta ya madini ambapo mpaka sasa kwa robo ya kwanza,jumla ya mizani 37 zimehakikiwa na kukidhi vigezo kwa mujibu wa Sheria yaVipimo Sura 340 na zinafaa kutumika katika uuzaji na ununuzi wa madini,”amesema Ikula.

Vilevile, ameeleza kuwa Mkoa wa Geita una jumla ya masoko kumi (10) ya kuuziana kununulia dhahabu ambayo ni Geita mjini, Katoro, Chato, Lwamgasa, Nyarugusu, Mbogwe, Bukombe, Nyang’wale, Mgusu na Nyakagwe.

Amedadavua kuwa, kutokana na uwepo wa masoko hayo, WMA hufanya kaguziza kushtukiza mara kwa mara kwa lengo la kujiridhisha kama vipimo vinatumikakwa usahihi ambapo kwa mtumiaji yeyote ambaye hubainika kuchezea vipimohuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura 340.

Naye Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa WMA, Bw. Paulus Oluochiamewahimiza wananchi kutembelea banda la WMA katika maonesho hayo iliwapate elimu ya vipimo pamoja na ushauri wa kitaalamu kuhusu vipimombalimbali.

Oluochi amesema kuwa, inapotokea mtumiaji yeyote wa vipimo akapatachangamoto yoyote anapaswa kuwasiliana na ofisi ya WMA iliyopo karibu iliaweze kupata msaada kwa haraka akifafanua kuwa ofisi za WMA zinapatikanakatika mikoa yote Tanzania Bara au atoe taarifa kwa namba ya bure ambayo ni0800 110097.
Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Geita Bi. Eva Ikula akitoa ushauri wa kitaalamu kwa mdau katika maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya madini Mkoa wa Geita.
Afisa Vipimo Mkoa wa Geita Bw. Tumaini Anyitike (katikati) akieleza umuhumu wa kutumia vipimo sahihi katika ufungashaji wa bidhaa kwa wajasiriamali waliotembelea banda la WMA katika maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya madini Mkoa wa Geita.
Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Mohamed Gombati (kulia) akikabidhiwa zawadi na Meneja wa WMA Mkoa wa Geita Bi. Eva Ikula mara baada ya kutembelea banda hilo katika maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya madini Mkoa wa Geita na kupata elimu ya vipimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...