Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mara.
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema mkakati wa Serikali katika miaka mitano ijayo ni kuendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kufungua fursa mbalimbali za Uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Musoma Mjini mkoani Mara ,Mgombea Urais Dk.Samia ameeleza kuwa mengi yamefanywa na Serikali miaka mitano iliyopita katika sekta mbalimbali lakini katika miaka mitano ijayo yale ambayo hajafanyika yanakwenda kutekelezwa kupitia Ilani ya Uchaguzi mwaka 2025-2030.
“Kwa upande wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi mgombea wa Musoma mjini amesema kinachokosekana ni uwezeshaji wananchi kiuchumi na hiyo ni kazi tunayokuja kuifanya.Serikali inakuja na mradi wa kujenga stendi na masoko nchi nzima ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara ndogondogo waweze kufanya kazi zao
“Lakini kupitia mfuko wa halmashauri wa asilimia 10 ambao tumeugawa kwa makundi ya wanawake ,vijana na wenye ulemavu nayo hiyo ni fursa nyingine ya kuwezesha wananchi kiuchumi.Wakati nazindua kampeni nilisema tutaanzisha mfuko wa wafanyabiashara ndogondogo ambao utaanza na Sh.bilioni 200.
“Hivyo kijana jipange ujue unataka kufanya biashara gani, stendi tunajenga, masoko tunajenga ,mifuko ya kukuwezesha ipo hivyo sema unataka kufanyabiashara gani
“Kuwmbwa zaidi tumesema katika Ilani mpya tunakwenda kurasimisha biashara ndogondogo zitambulike,ziwe rasmi ili waweze kufaifika kama wafanyabiashara wengine wanavyofaifika.”
Dk.Samia amesema kuwa katika kuwawezesha wananchi Serikali pia imekuja na mfumo wa ruzuku katika kilimo na pembejeo na kwa maeneo mengine dawa za kuua magugu na kupulizia inatolewa bure
Amesema kwa upande wa ufugaji Serikali imetoa chanjo ya mifugo kwa ruzuku na chanjo ya kuku ni bure kabisa wakati katika umeme gharama za kuunganisha umeme sio chini ya Sh.400,000 katika maeneo yote lakini kwa wale wa vijijini ambao uwezo wa mdogo wanaunga umeme kwa Sh 27000 peke yake na fedha iliyobakia inatolewa na Serikali
"Yote hii ni kuwezesha watu wetu ,mtu anatamani kuwa na umeme hana uwezo toa Sh.27000 unapata umeme, anatamani kufanyabiashara mifuko ipo fanyabiashara.
“Tunatoa elimu bila ada darasa la kwanza mpaka kidato cha sita,fedha.ambayo baba au mama angeitoa kulipia ada inabaki mfukoni kwake kote huko ni kukuwezesha mwananchi kiuchumi.
“Katika Ilani iliyopita na hii mpya kuna makundi ambayo hayalipii huduma za afya hiyo nayo ni kumnusuru mwananchi kulinda afya yake, fedha aliyokuwa atumie kulipa gharama za matibabu ya afya inabakia mfukoni kwake.Huko kote ni kumuwezesha mwananchi kiuchumi.”
Akieleza zaidi Dk.Samia amesema pia Serikali inaendelea na mkakati wa kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga skimu ,kujenga mabwawa na kwa upande wa uvuvi imefanya mengi zaidi ikiwemo ufugaji samaki kwa mabwawa na vizimba ambapo vijana wanafanya kazi ya ufugaji samaki.
"Tunaamini kupitia sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji baadae italeta maendeleo ya viwanda na ndio maana tumsema kila Wilaya kutakuwa na kongani za viwanda ambazo zitaongeza thamani ya kile ambacho kinafanyika katika wilaya husika kwa kuongeza thamani ya mazao ya kilimo,uvuvi na hata madini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...