*Aahidi kuendelea kuupanua Uwanja wa Ndege ,kukagua bandari,ujenzi wa SGR

*Awaomba wananchi Mkoa wa Mara Oktoba 29 waipigie kura CCM iendelee na kazi 


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mara

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mara kuwa Serikali itaendelea na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara,reli,Uwanja wa ndege na reli kwani ndio inayowezesha Mkoa huo kukua kiuchumi.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi and wa Musoma Mjini mkoani Mara alipokuwa katika mkutano wa kampeni kuomba kura kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu, Dk.Samia amesema katika Mkoa huo Serikali imejenga miundombinu ya barabara na kazi bado inaendelea.

“Kwa upande wa miundombinu ambayo ndio inawezesha kukua kiuchumi hapa Mkoa wa Mara barabara tumeanza kujenga na nyingine ziko katika Ilani mpya.Pia tunatambua Mara kuna haja uwanja wake wa ndege kufanyiwa kazi ya upanuzi.

“Tumetoa fedha kuutanua uwanja wa ndege awamu ya kwanza lakini tutauendeleza mpaka ufikie viwango vya kutua ndugu kubwa ambazo zitakuja Mara kibiashara.”

Kuhusu bandari Dk.Samia amesema kuna bandari za zamani zimeachwakutumika na nyingine zinatumika hivyo mkakati wa Serikali ni  kuendeleza usafiri katika maji hivyo bandari ambazo hazitumiki zitafufuliwa zote.

“Kwasababu tayari pale Mwanza tumejenga meli kubwa ambayo itasafiri kuja hapa Musoma na kisha kwenda kwa majirani zetu Uganda.Kwahiyo bandari lazima tuzifufue zipokee meli kubwa ili biashara iweze kushamiri ndani ya nchi yetu ndani ya mikoa yetu.

“Kubwa zaidi  ni mradi wa reli ya SGR ambayo itatoka Bandari ya Tanga na tuunganishe na moja ya bandari kubwa tutakazojenga hapa Musoma.Reli ya SGR itatoka  Tanga itapita Kilimanjaro , Arusha na kisha Musoma.Kwahiyo reli hii inakuja na Mapinduzi ya kiuchumi ndani ya mkoa huu.”Amesema Dk.Samia mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa huo.

Kutokana na maelezo hayo na mengine ambayo ameyaeleza kuhusu

Mkoa huo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi Oktoba 29 mwaka huu ambayo ndio siku ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi na kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.

“Ndugu zangu wana Mara twendeni tukachague Chama Cha Mapinduzi ili haya niliyoyasema tuje tuyafanyie kazi,ombi langu kwenu najua ndani ya Mkoa wa Mara kuna watu wamenuna na katika kununa kwao wanataka waikomoe  CCM.

“Nataka kuwaambia CCM haikomoki na katika kuhakikisha hilo niwaombe tarehe 29 mwaka huu tutoke wote kwa pamoja tuchague Chama Cha Mapinduzi .

“Ukipeleka huko unakoshawishiwa umepeleka kura yako kwenye ziro na kama mtatoa jimbo kwa huko hilo jimbo lina ziro lakini ukija huku kwetu CCM mambo yako katika  Ilani ambayo inaeleza kila kitakachofanyika ndani ya wilaya .

“Nendeni kachagueni CCM ambayo kazi zetu ziko katika Ilani  ya uchaguzi mkuu ambayo tumeiweka katika vitabu viwili kikubwa kinachoelezea yatakayofanyika nchi nzima na kitabu kidogo cha Ilani kinachoelezea  yatakayofanyika kwa kila Mkoa.Hivyo tupeni kazi tukajenge utu wa mtanzania,utu wa mwana Mara ,utu wa mtu wa Musoma.”









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...