Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga, amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura Oktoba 29 katika Uchaguzi Mkuu na hakuna mtu yoyote wa kuvuruga uchaguzi au kufanya maandamano.
Bananga alitoa wito huo, katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM Kata ya Kigamboni, Dar es Salaam, juzi.
Alisema wasiwe na wasiwasi wataenda kupiga kura kwa amani na kurudi katika makazi ya kwa amani na kusubili matokeo amani.
"Kwanza niwahakikishieni hakutakuwa na maandamano, kwani maandamano hayawezi kuratibiwa Marekani alafu yafanyike nchini Tanzania, hakuna mtu atakayejitokeza kufanya maandamano", alisema.
Pia Bananga amemtaka mgombea udiwani Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa kuhakikisha, wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wanapatiwa mikopo ya asilimia 10, kutoka Halmashauri.
Alisema mikopo hiyo ni kwaajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambao hawana dhamana za kukopesheka na mabenki.
"Hakikisha wanaopata mikopo ni wanawake wa kawaida ambao hawana dhamana za kepeleka kupata mikopo, wapeni hawa wakazikwamue familiaza kwa kufanyabuashara ndogo ndogo, alisema.
Kwa upande wa kata hiyo, Msawa aliwaomba wananchi wa Kata ya Kigamboni na Watanzania kupigia kura nyingi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kwasababu amefanya mambo mengi mazuri ndani kipinda cha miaka minne ya uongozi wake.
"Mama Samia alipoingia madarakani ndiye imejengwa Shule ya Sekondari Paul Makonda ya ghorofa yenye thamani ya Sh. zaidi ya Bilioni 1.5, ametofedha kwaajili ya elimu bure kwa watoto wetu, meza na madawati kwa shule za sekondari. Tulikuwa na zahanati ndogo lakini sasa amejenga kituo cha afya", alisema.
Pia Msawa alisema katika uongozi wa Dk. Samia, amewapa gari la kubeba wagongwa, mashine ya X-ray, ametoa fedha nyingi za ujenzi wa miundombinu ya barabara zote za kata hiyo.
Aidha, Msawa alimuhakikishia Bananga kuwa endapo atachaguliwa ataendelea kusimamia vizuri fedha za mikopo kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kama alivyofanya kipindi kilichopita.
"Mwenezi kuhusu mikopo ya asilimia 10 ya vijana, wanawake na wenye ulemavu niliisimamia vizuri, kuanzia kwa vijana wa bodaboda, mamalishe na wengine wote, katika kata yangu niliyoingoza hatukuwa na tatizo kwamakundi hayo kupata mikopo, tuko vizuri", alisema.


.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...