Na Emmanuel Masaka,Michuzi TV

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, ametoa rai Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 Oktoba, mwaka huu huku akisisitiza kufanya hivyo ni haki yao ya kikatiba.

Abdulla ametoa rai hiyo wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba, kwenye viwanja vya ZSM Mjimbioni.

Amesema, “Watanzania jitokezeni kwa wingi mkapige kura, kwani kupiga kura ni haki yenu ya msingi kama raia wa Tanzania.”

Aidha,Abdulla amewataka wananchi kuwapa kura wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi mbalimbali, ili kuendeleza maendeleo yaliyofikiwa na Serikali chini ya uongozi wa chama hicho.

Awali Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Abdallah Kassim, kupitia tiketi ya CCM, ameeleza kwamba katika Jimbo la Mtambile ni sherehe za ushindi ndizo zinaendelea na hakuna dalili zozote za maandamano.

Pia amesema wananchi wa Jimbo la Mtambile wako tayari kumpa kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Akihitimisha hotuba yake,Hemed amewataka Watanzania wote kuendelea kuilinda na kuithamini amani ya nchi kama walivyoikuta, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo na ustawi wa taifa.

“Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kubaki nchi ya amani. Tuihifadhi amani hii tuliyoirithi kutoka kwa waasisi wa taifa letu, kwani bila amani hakuna maendeleo,” amesema Hemed.

Kampeni hizo za CCM katika Jimbo la Mtambile zimefungwa rasmi kwa amani, hamasa kubwa na mwitikio chanya kutoka kwa wananchi.





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza wakati wa kufunga kampeni Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akimnadi na kumuombea kura kijana Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtambile, Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Abdallah Kassim,
(Picha  zote na Emmanuel Massaka,Michuzi Tv)











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...