Na Mwandishi wetu.
Siku chache baada ya uzinduzi rasmi wa programu maalum ya Konekt Umeme, Pika kwa Umeme uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kutekeleza kwa mafanikio makubwa zoezi la kuwaunganishia wananchi umeme pamoja na kuwapatia kwa mkopo majiko ya umeme kwa ajili ya kupikia.
Programu hii, inayotekelezwa nchi nzima, ni sehemu ya Mpango wa Kitaifa wa Nishati (Energy Compact) unaolenga kuwaunganishia umeme wananchi milioni 8.5 ifikapo mwaka 2030, sawa na takribani wateja wapya milioni 1.7 kila mwaka.
Wananchi katika mikoa mbalimbali wameanza kunufaika na mpango huu tangu kuanza rasmi kwa zoezi hilo tarehe 15 Oktoba 2025. Wengi wameeleza kufurahishwa na mpango huo, hususan kwa kuwa unalenga kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kupata majiko ya umeme kwa utaratibu wa mkopo, hali iliyowasaidia kuanza kutumia nishati safi na salama kwa kupikia.
Aidha, wananchi hao wameiomba TANESCO kuhakikisha majiko yanayotumia umeme kwa kiwango kidogo yanapatikana kwa wingi kutokana na mahitaji makubwa yaliyojitokeza.
Wameeleza kuwa matumizi ya umeme kwa kupikia ni nafuu na salama zaidi ikilinganishwa na nishati nyingine kama mkaa na kuni, hivyo ni muhimu elimu ya matumizi ya umeme jikoni ikaendelea kutolewa kwa wananchi.
Utekelezaji wa mpango huu unafanyika kwa kushirikiana na Mradi wa Modern Energy Cooking Services (MECS) chini ya Serikali ya Uingereza, ambapo wateja wapya waliounganishiwa umeme wataweza kulipia majiko hayo kwa awamu kupitia manunuzi yao ya umeme.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...