-“Usiku wa Mabingwa” Waadhimisha Ubora, Shauku na Miaka 25 ya Huduma
Vodacom Tanzania PLC imehitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa hafla ya utoaji wa tuzo, iliyobeba kaulimbiu ya “Usiku wa Mabingwa.” Hafla hiyo iliwaenzi wafanyakazi wanaohudumia wateja na timu za usaidizi ambao kwa kujitolea kwao bila kuyumba, wameendelea kuunda historia ya Vodacom katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.
Akitoa hotuba kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Vivienne Penessis aliwasifu wafanyakazi wa usaidizi kama mhimili wa mafanikio ya chapa ya Vodacom, “usiku wa leo tumekusanyika kuwaenzi mashujaa wa safari yetu ya huduma kwa wateja. Uaminifu wenu, shauku yenu na uvumilivu wenu ndio sababu Vodacom inaendelea kuongoza katika ubora wa huduma.”
Akielezea safari ya miaka 25 ya Vodacom, Penessis aliongeza, “urithi wa Vodacom haupo tu katika teknolojia, bali uko katika mahusiano ya kibinadamu tuliyojenga kwa muda. Na watu tunaowaenzi leo wamekuwa sehemu muhimu ya ukuaji wetu si kwa idadi tu, bali kwa uaminifu, sifa na matokeo chanya.”
Kwa upande wake, Belinda Wera, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidijitali, alisisitiza kuwa hafla hiyo inalenga kutambua juhudi za timu zinazowahudumia wateja moja kwa moja pamoja na wale wanaofanya kazi nyuma ya pazia.
“Tuzo zilizotolewa usiku huu ni zaidi ya utambuzi ni taswira ya utamaduni wa Vodacom, kama unavyooneshwa na watoa huduma wetu katika maeneo yote ya huduma kama vile kituo cha huduma kwa wateja (Call Centre), ofisi inayohudumia kutoka ndani (Back office), msaada wa moja kwa moja katika maduka, pamoja na timu za msaada wa mtandao na TEHAMA.”
Usiku wa Mabingwa uliwaenzi wafanyakazi wa Vodacom wanaoishi kwa vitendo nguzo kuu za kampuni hiyo, wanaounganisha timu kufanikisha matokeo, wanaobuni kwa ujasiri kwa ajili ya kesho, wanaojifunza haraka kupitia majaribio na wanaojenga uaminifu wa wateja kwa kutoa huduma bora.
Usiku huo pia ulijumuisha vipaji vya ubunifu, ambapo wafanyakazi wa Vodacom walitoa burudani kupitia muziki, vichekesho, ushairi na amidi wa hafla (MC’s) ikiashiria utofauti na ubora unaozidi huduma kwa wateja.
Katika hafla hiyo, jumla ya tuzo 38 zilitolewa kutambua mchango wa kipekee kutoka kwa timu na idara mbalimbali. Hii ilijumuisha tuzo 37 za mtu binafsi na tuzo 1 ya timu iliyojitokeza katika utendaji wa kipekee.

Mkurugenzi wa Sheria wa Vodacom Tanzania Plc, Olaf Mumburi (kushoto), akikabidhi tuzo kwa mfanyakazi Francis Baragwiha (katikati) wakati wa hafla ya "Usiku wa Mabingwa", iliyosherehekea wafanyakazi waliochangia mafanikio ya kampuni hiyo wakati wa kilele cha wiki ya huduma kwa wateja. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja na Kidigitali, Belinda Wera. Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...