Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bw. Albert Machua, wakati wa kikao kazi cha kuwakaribisha Taasisi ya Watu wenye Ulemavu Peace Life for Persons with Disability Foundation (PLPDF).

 

Bw. Machua amesema mradi huo unalenga kuwawezesha wasichana, wanawake na vijana wenye ulemavu kiuchumi na kimaendeleo, ambapo utekelezaji wake utaanza katika wilaya za Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa PLPDF Bi. Sophia Mbeyela amesema mradi huo utatoa elimu ya maisha, ujasiriamali na uelewa kuhusu mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu (ADB), huku wakitarajia kuwafikia zaidi ya watu wenye ulemavu mia moja ili kuongeza uhamasishaji katika jamii.

 

Naye Wakili Gidion Mandesi ameeleza kuwa mkataba wa ADB unaelekeza ulinzi na haki za watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali, ikiwemo upatikanaji wa huduma, elimu na fursa sawa katika jamii.









Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...